Saturday, August 8, 2009

TUMUENZI MUNGU KWA NJIA YA GOSPEL

Anaitwa HLLEN JUMA NJAMA, mwimbaji mwingine wa muziki wa injili anayechipukia kwa kasi. Akiwa na undugu na mwimbaji maarufu katika muziki huo, Christine Shusho, Hellen hivi sasa anatamba na albamu iitwayo Yesu Niokoe yenye jumla ya nyimbo nane ambazo ni Yesu Niokoe, Sindalile, Nalia na nyingine. Kazi hiyo inatarajiwa kuzinduliwa Agosti 30 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Msimbazi ambapo Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecella, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi. Vilevile watakuwepo wabunge wengine kama Idd Azzan, Aziza Ally pamoja na Al-Shalmar Kweygir. Wapenzi wa Gospel ni wakati mwingine wa kumtukuza Mungu kupitia mwimbaji huyu.

No comments: