Monday, August 17, 2009

WIKIENDA SHOWBIZ!

ALIKIBA KWA KULA USIPIME!
Good sound, beat and rhythm ni vitu ambavyo vinaipaisha singo mpya ya fundi wa vocal za kubembeleza Bongo, Ali Saleh Kiba ‘Alikiba’.

Traki inatambaa kwa jina la Napenda Kula, ndani yake ‘bwa mdogo’ hajasumbua kichwa kutoa mistari yenye meseji ila alichokifanya ni next level. Mzigo umesimama na ukiusikiliza unavunja mbavu.

Sikia; alivamia sherehe bila kualikwa, akanawa na kuanza kuchota pilau kwa mikono, tonge nyama, tonge nyama, waungwana wakaona dogo anawazingua, spidi kali wakati siyo mhusika, wakamtoa baruti.

Unadhani walipomfukuza palikalika? Alienda kununua mayai, bila shaka ni viza, sherehe ikavurugika, dogo aliwachachafya vibaya na mayai. Mzigo umesimama. Upo vizuri, chapa mwendo, one day utaitwa mfalme.

########################################################

TEARS ON VALENTINE
Itabadilisha movie industry Bongo
Filamu ambayo inarekodiwa hivi sasa, Tears on Valentine’s Day inatajwa kwamba itakuja na vitu tofauti ambavyo waandaaji wengi wa Bongo huvikwepa wakati wa kuandaa muvi zao kutokana na kukwepa gharama au kuzidiwa ujanja na teknolojia.

Mkurugenzi wa Filamu katika Kampuni ya Tollywood Movies inayoandaa filamu hiyo, Hamie Rajab amenong’ona na Abby Cool & MC George over the weekend kwamba zoezi zima la kutengeneza muvi hiyo limezingatia maeneo mengi ya kisasa.

“Tunataka kuonesha kuwa Tanzania tunaweza kuwa mbele zaidi, muhimu ni kujipanga. Wasanii tuliowachukua kwa ajili ya kurekodi ni wa kiwango cha juu sana, mandhari inayotosheleza mahitaji ya stori ya filamu na picha za kiwango cha juu,” alisema Hamie na kuongeza:

“Waandaaji wengi hukwepa vitu fulani fulani wakati wa kurekodi filamu zao kutokana na gharama au teknolojia lakini ndani ya Tears on Valentine’s Day utaona maendeleo ya kiteknolojia ambayo Tollywood inayo na tumekubali kuingia gharama kubwa ili kutoa kitu bora.”

##################################################

Samantha
Sisqo
Eminem

SAMANTHA MUMBA: KUMBE AMEWAHI KUJIKUNJA NA EMINEM!
Yupo kimya sana hivi sasa lakini Ebwana Dah! Imeona si kihivyo, that’s why ikaingia kunako intaneti na kufunua orodha ya njemba ambazo yeye amewahi kutoka nazo kimahaba.

Kwa mujibu wa kile ambacho tume-capture kwenye site inayodili na ishuz za uhusiano wa mastaa mbalimbali wa mtoni, Samantha amekwishajituliza kwa vidume watano katika mtindo unaokuijia hapo chini.

Inawekwa hivi, mwaka 1998 mpaka 2003 alikuwa amejituliza kwa Mark Henderson lakini mwaka 2000 alicheza pembeni na kujikunja na Colin Farrell, 2001 alikubali kupumzika kwa kichaa Bruce Mathers III ‘Eminem’ kabla ya mwaka 2005 kuangukia kwa Charles Porter ambaye yupo naye mpaka sasa.

Hata hivyo, mwaka 2005 aliwahi kutuliza ‘mizuka’ kwa Sisqo ambaye walichangamshana damu kwa muda.
#############################################

...coming soon

compiled by mc george

No comments: