Sunday, September 13, 2009

WIKIENDA SHOWBIZ!

Snoop Dogg Hawa ndiyo mademu aliokuwa nao
The Tuff Wallet MC, Snoop Dog Dogg ndiye staa anayepandishwa kwenye kizimba cha Ebwana Dah! Halafu kinachofuata ni kuweka hadharani orodha ya watoto aliopumzika nao.

Mtandao wa kiwanja ambao ume-specialize katika eneo la staa gani anatoka na nani, unamtaja Chavonne Hodges kama nambari moja kujikunja na Snoop. Warembo Izabela, Aleksandra, Monika Okapiec na Karrine Steffans nao wanawekwa kwenye orodha hiyo ingawa hakuna maelezo ya kina ni lini walijichangamsha naye.

Mwaka 1997 inaelezwa kuwa ndiyo Snoop alianza ku-make issues za romance na Shantay Taylor Broadus, hivyo kufanya jumla ya watoto aliofanya nao safari ya bed the stage kufikia sita.

Jina lake kamili ni Cordozar Calvin Broadus, pia anatambulika kwa majina kama Snoop Doggy Dogg, Bigg Snoop Dogg na Tha Doggfather. Umri wake ni miaka 37, alizaliwa Oktoba 20, 1971 na urefu wake ni futi 6 3½. Dini yake ni Mwislamu, alisoma Long Beach Polytechnic High School, Long Beach, California.
******************

Irene Sanga: Is back 2 da game na traki mbili mpya
Sterling wa wimbo Salamu kwa Mjomba, Irene Sanga amesema kuwa hivi sasa anakuja upya na ngoma mbili ambazo zitathibitisha uwezo wake katika kiwanda cha muziki.

Mbali na hilo, pia Irene alisema kuwa hivi sasa hana bifu na mwanamalenga, Mrisho Mpoto ‘Mjomba’ kwa kuwa ule mgogoro wa wimbo Salamu kwa Mjomba ulishakuwa settled na amani inatawala kati yao. “

Tulimalizana na Mpoto kwa sababu aliutumia wimbo wangu kwenye albamu yake, nisingependa kuongelea sana ishu hiyo,” alisema Irene.

Baada ya kuipotezea ishu ya Salamu kwa Mjomba, Irene alisema kuwa fans wake wakae tayari kwa kuwa anakuja na nyimbo mbili za kiwango cha juu ambazo alizitaja kwa majina kuwa ni Never Give Up na Msimu Umeshafika. Alisema:

“Never Give Up nawazungumzia wanawake na nawataka wawe majasiri na wasikate tamaa. Video za nyimbo zote mbili nimezifanya kwenye studio yangu ya Ukala Production.”
****************
Madhila: Inadondoka kitaani kwa kishindo leo
Ilisubiriwa kwa muda mrefu lakini leo utepe unakatwa, filamu ya Madhila II inaingia mtaani tayari kabisa kuwapa kitu sahihi wadau wa kiwanda cha muvi Bongo. Filamu hiyo ambayo haihitaji maelezo mengi kwa sababu imekuwa gumzo kwa miezi kadhaa sasa mfululizo, itauzwa katika DVD, VCD na VHS.

Filamu hiyo itakayozungushwa mtaani kwa ufanisi wa hali ya juu na kampuni mkombozi wa vipaji nchini, Tollywood Movies, inakuja na picha kuwa mtu akiwa mlemavu haina maana kwamba maisha ndiyo yamefikia kwenye ukomo.

Mwendesha filamu wa Tollywood Movies, Hammie Rajab ,alisema kuwa kukamilika kisha kuingia sokoni kwa filamu ya Madhila II ni ushahidi kuwa ulemavu ni changamoto tu lakini maisha yanaendelea. Hammie alisema kuwa mhusika mkuu wa filamu hiyo, Salum Mbwana ‘Salu’ ambaye kwa uhalisia ni mlemavu ameonesha njia kwa wengine wenye matatizo kama yake ambao badala ya kupigania maisha wamekuwa wepesi wa kukata tamaa.


“Anafundisha vitu viwili, mosi, Salu ndiye mtayarishaji na muigizaji wa filamu hiyo, kwahiyo ameipigana mpaka kuisimamisha na leo tunaizungumzia kuingia mtaani. Anastahili kuwa mfano wa kuigwa na wenzake waliokata tamaa au wanaofikiria kufanya hivyo.

“Pili ni ujumbe alioufikisha kupitia filamu kwamba jamii yetu imekuwa ikiwanyanyapaa walemavu bila kuzingatia kuwa nao ni watu wanaostahili heshima na utu kama ambavyo Salu alivyofanyiwa lakini mwisho wa siku alionesha kuwa inawezekana.

“Tatu ambalo ningependa nigusie ni kuwa watoto ambao wataonekana ni wa Salu kwenye maigizo, wale ni watoto wake kabisa, hivyo anazidi kuthibitisha kuwa kumbe hata mlemavu anaweza kuongoza familia yake,” alisema Hammie. Usikose nakala yako kuanzia leo.
*************************************
Wape shavu A.Y, Shaa MTV
Awadi za MTV Africa Music (MAMA) still on air na siyo stori kuwa Ambwene Yesaya ‘AY’ na Sara Kaisi ‘Shaa’, Wabongo pekee waliopata ngekewa ya kuwa nominees.

AY anachuana na wakali wengi wa kiwanja akiwemo Jigga katika tuzo ya Msanii Bora wa Hip Hop na Shaa anaparurana na wasanii wa mataifa mengine katika tuzo ya Msanii Bora Anayechipukiakuja. Wanaweza kushinda ikiwa tu hautobana kuwapa shavu, kumchagua AY andika neno BHH AY kwenda namba 0789 777 333 na Shaa unaandika BNA SHAA kwenda namba 0789 777 333. Unaweza kupiga kura mara nyingi uwezavyo ili kuipa heshima Tanzania katika eneo la muziki.

********************
Black, FA Wanahitaji sapoti yako
Tuzo za Channel O zinaendelea kuchukua nafasi, Nicolas Haule ‘Black Rhino’ (pichani) na Hamis Mwinjuma ‘FA’ wamo ndani ya nyumba, hivyo Mtanzania unaweza kuwa daraja la wadogo zetu hao kushinda na kurudi Bongo wakiwa na full respect.

Black kupitia wimbo wake Black Chata, ametajwa kwenye categories mbili, Video Bora Afrika Mashariki (Most Gifted East Afrika Video) na Video Bora ya Hip Hop (Most Gifted Hip Hop Video). FA pia kupitia ngoma yake Naongea na Wewe ambayo amefanya kolabo na Ambwene Yesaya ‘AY’ ametajwa kwenye vipengele viwili, Video Bora Afrika Mashariki (Most Gifted East Afrika Video) na Wimbo Bora wa Kushirikiana (Most Gifted Group a.k.a Duo).

Utaona kwamba Black na FA wanakamuana pua kwenye category moja ambayo ni Video Bora Afrika Mashariki; lakini siyo ishu, muhimu hapa ni kuleta heshima home. Unawezaje kupiga kura? Video Bora Afrika Mashariki, kwa Black tuma SMS yenye maneno 13E au FA 13B kwenda namba +27839208400. Video Bora ya Hip Hop, unampigia kura Black kwa kuandika SMS yenye maneno 10F na unaituma kwenda nambari +27839208400, wakati ili FA ashinde Wimbo Bora wa Kushirikiana, unaandika 4E kwenda +27839208400.
*****************************
compiled by mc george

No comments: