Friday, February 19, 2010

IJUMAA SHOWBIZ!


Kutoka TMK Family, sura mbili ambazo zinafanya vyema kupitia mradi wa muziki wa kizazi kipya, Amani James Mhe. Temba na Said Juma a.k.a Chegge zimetangaza vita ya kupambana na mashabiki wao.

Wakipiga stori na ShowBiz kwa nyakati tofauti wasanii hao walisema kuwa, kinachofanyika siyo vita ya kutoana damu, ni ya maneno ambayo yanapatikana ndani ya ngoma zao ikiwemo ‘Mkono mmoja’ ambayo inatambulisha albamu yao yenye jina hilo hilo, ‘Vita mbele’.

Stori nyingine waliyopiga na safu hii ni kwamba hivi sasa wanagonga ‘projekti’ ya pamoja baada ya Chegge kutupa ‘street’ albamu yake, ‘Karibu kiumeni’ huku akiwa anafanya poa na mzigo wenye jina la ‘Mambo bado’ uliompa shavu Judith Wambura Mbibo a.k.a Lady Jaydee.

“Ndani ya Mkono mmoja tumempa shavu Wahuu kutoka Kenya, Vita Uwanjani ni projekti ambayo tumeifikiria fasta na kuigonga kisha kukamilisha albamu kwakuwa mashabiki walionesha kutamani sisi wawili kupiga ishu pamoja. Kitakachofuata baada ya mchongo huu ni kuusimamisha mzigo wa kundi letu, TMK Wanaume Family,” alisema Temba ambaye hivi sasa anajiita ‘Washa Washa’.

Ishu nyingine kuhusu washkaji ni kwamba, siku kadhaa zilizopita walimdondosha Bongo Wahuu ambaye amesimama vyema kwenye ngoma yao, Mkono mmoja kwa ajili ya kukamilisha video ya kazi hiyo kupitia Kampuni ya Visual Lab na mpaka tunakwenda mitamboni tayari mzigo ulikuwa umekamilika, kinachosubiriwa ni kuupeleka on air kupitia vituo kadhaa vya runinga.

Kwa maoni zaidi kuhusu washkaji na safu hii cheki na sisi kupitia 0787 110 173.

*********************************************************

Hemed apata mchumba, yuko tayari kuvuta jiko
Staa wa filamu na muziki Bongo, Hemedy Suleiman amesema na ShowBiz kuwa hivi sasa yupo tayari kuoa kwakuwa mchumba ameshampata.

Hemedy, alicheki na safu hii kwa njia ya SMS wikiendi iliyopita kuwa ameamua kutafuta mchumba wa kuoa ili kuondokana na kashfa ya kuchukua wake za watu ambayo imevumishwa na kumchafulia wasifu wake.

“Ebwana nimeamua kutafuta mchumba na soon nitamuweka wazi ili watu wajue! Skendo ya kutembea na wake za watu inaharibu file langu kwa kuwa hakuna ukweli kuhusu hilo. Maisha yangu ya tabu na daily napewa vitisho. Nimechoka,” alisema Hemedy.

***************************************************************
Baada ya kumsoma mchawi wake H. Baba aanza kazi upya
Wiki kadhaa zilizopita safu ndugu na hii, Abby Cool & MC George Over the weekend inayopatikana ndani ya Gazeti la Ijumaa Wikienda ilikudondoshea ishu ya msanii Hamis Ramadhani a.k.a H. Baba aliyedai kurogwa na msanii mwenzake (jina tunalipotezea) kitu kilichomfanya apotee kunako game hiyo.

Katikati ya wiki hii mchizi alidondoka ndani ya ShowBiz na kuchana kwamba, hivi sasa yuko poa na tayari amerudi mzigoni upya akijiandaa kusukuma hewani ngoma yenye jina la ‘Umeshaniumiza’ ikiitambulisha albamu yake mpya, ‘Goma la Uswazi’ ambayo tayari wadosi wameshaikamata.

“Mwaka ndiyo umeanza na mimi nalianzisha kwa staili hii baada ya kutoka home Mwanza kucheki afya yangu. Albamu ina ngom 8 zikiwemo Fukara, Njoo kwa wema, Kinachoniumiza, Goma la Uswazi na nyingine kibao. Nimewapa mashavu wasanii kama Tundaman, Hussein Machozi, Bushoke na wengine kibao,” alisema H. Baba.

compiled by mc george

No comments: