Friday, February 26, 2010

IJUMAA SHOWBIZ!

A.Y aipeleka Kings & Queens redioni
The Commercial Rapper, Ambwene Yesaya ‘A.Y’ ameipeleka traki yake ya Kings & Queens redioni lengo likiwa ni kuifanya isikike kwa wengi.

Awali, ngoma hiyo ya A.Y iliachiwa kideoni pekee lakini baada ya kuona kuwa redio zina nafasi kubwa ya kuujuza umma wa Watanzania what’s going on, ameamua kuitupia na huko ili wadau wengi wainyake.

A.Y alisema na Showbiz juzi, Jumatano: “Ngoma yangu ya Kings & Queens imesukwa na Harmy B pale B. Hitz Records. Humo ndani nimewasifia wanawake weusi kwa sababu naamini ndiyo wanawake wazuri hapa duniani, so najivunia kuzaliwa kwenye bara la wanawake weusi.”
********************************************

Mashujaa wa Haiti na Around the World Tour
Mastaa waliojitoa kupiga mzigo kwa ajili ya kukusanya mshiko wa kuwasaidia waathirika wa Tetemeko la Ardhi katika Kisiwa cha Haiti, wameweka plani za kuizunguka dunia ili kuchangisha fedha.

Mashujaa hao, Kanye West, Miley Cyrus, Justin Bieber, Jamie Foxx, Jeff Bridges, Vince Vaughn, Usher, T-Pain, Bizzy Bone, Kid Cudi, LL Cool J, Snoop Dogg, Drake, Mann, Mya, Nipsey Hussle, Busta Rhymes, Swizz Beatz, Lil Wayn na wengine kibao, watasafiri Around the World hasa baada ya singo yao waliyoimba pamoja kusaidia maafa hayo kufanya vema.

Katika wimbo huo, mastaa hao wamerudia track ya We are the World ambayo ilifanywa miaka hiyo na wakali Michael Jackson, Steve Wonder, Lionel Rich na wengineo kwa lengo la kusaidia watoto wa Bara la Afrika kutokana na matatizo ya vita. Awali mashairi ya pini hilo yaliandikwa na marehemu Michael Jackson akishirikiana na mkali wa kulalamika Lione Richie.

Mpaka sasa, mashujaa wa Haiti wamekwishauza nakala nyingi za wimbo huo kiasi cha kufikia hadhi ya Platinum lakini wanadhani wakiizunguka dunia wakifanya kazi ya hisani, kwa kufanya shoo ili fedha zitumike kukuza mfuko wa kuwasaidia waathirika, litakuwa ni jambo bora zaidi.
******************************************

SHAA AUKAMIA MBAYA 2010
Staa anayevaa jezi ya Wanamuziki wa Kizazi Kipya, Sarah Kaisi ‘Shaa’ ameukamia mbaya mwaka huu wa 2010 kutokana na mikakati yake ya kujaza gunia ikiwa ni pamoja na kuipua albamu yenye moto mkali.

Shaa aliimegea Showbiz juzi kwa njia ya waya kuwa hivi sasa yupo very busy akishughulikia video za track zake mbili ambazo anatarajiwa kuziweka hewani muda si mrefu.
******************************************************
STEVE: Athibitisha yeye ni Special One katika R&B
Steven William Gambo a.k.a Steve wa R&B, once again amethibitisha kwamba yeye ni ‘Special One’ katika uwanja wa staili hiyo ya muziki Bongo, kwa kuachia traki yenye meno makali inayopenyeka vizuri masikioni, ngoma inakwenda kwa jina la One Love.

Before, Steve anayelelewa na Kampuni ya Zizzou Entertainment, alitamba na ngoma tamu isiyochuja, inayokwenda kwa jina la ‘Sogea Karibu’ akimshirikisha Dataz na baada ya hapo alinyamaza ingawa sauti yake ilisikika kwenye pini mbalimbali ambazo alishirikishwa.

Ndani ya ‘One Love’, Steve akiwa amesimama na Baby Boy, ameweza kuonesha kwamba yeye siyo tu fundi wa kuimba bali pia kuweka vionjo na ujumbe unaoendana na misingi ya R&B.

Steve alisema nasi last Wednesday: “Natoa ngoma za ukweli ili albamu yangu ikubalike. Mpaka sasa nimesharekodi traki sita bado nne kukamilisha 10. Wanangu Ngwair, Baby Boy, Squeezer, Dataz wameweka vocal katika nyimbo tofauti tofauti.”

*********************************************



Kalapina Atangaza kuwania udiwani ki’ndoni
Bongo Flava ipo ‘levo’ nyingine kwa sasa na wasanii wake ambao kipindi hicho wanaanza kusababisha walionekana ni ‘madogo lee’ nowdays wamepevuka na mawazo yao ni ya kiutu uzima, kamatia hii.

Mwana-Hip Hop mwenye harakati zenye uzani mkubwa Bongo, Kalama Masoud ‘Kalapina’ amejitosa kwenye ulingo wa kisiasa ikiwa ni pamoja na kuweka wazi azma yake ya kugombea Udiwani wa Kata ya Kinondoni, Dar.

Kalapina ameitonya Ijumaa Showbiz kuwa dhamira yake ya kuwania udiwani kwenye kata hiyo ni kushirikiana vema na wananchi ili kuindeleza kata hiyo kwa huduma mbalimbali za kijamii, kiuchumi, pia kuendeleza harakati za vijana katika Mapinduzi ya Kisiasa.

“Nawaomba wananchi wenzangu waniunge mkono ili tuendeleze harakati, muziki kama kawaida siachi, nitafanya siasa na muziki pamoja. Ijulikane kuwa sikuingia kwenye siasa kwa kukurupuka, bali naijua, pia wazee wamenishauri nigombee kwa sababu nakubalika sana kwenye kata yetu,” alisema Kalapina na kuongeza:

“Nagombea kwa tiketi ya CUF, mimi ni mwanachama wa CUF tangu mwaka 1999. Nataka nimpumzishe diwani wa sasa Michael Lupiana kwasababu siasa ya siku hizi inahitaji vijana wenye uwezo wa kusimamia mambo, kujenga hoja, kubuni na kutekeleza masuala yenye manufaa kwenye jamii, sifa ambayo mimi ninayo.”


compiled by Mc George/Ijumaa newspaper

No comments: