Tuesday, February 2, 2010

TIBA YA LISHE KWA WAGONJWA WA ANEMIA

Hakuna tiba bora kama chakula na kila ugonjwa una chakula chake kama tiba. Mgonjwa hulazimika kutumia dawa za hospitali pale hali inapokuwa mbaya na ugonjwa unapokuwa umefikia hali mbaya.

Hata hivyo, baada ya mgonjwa kujijua ugonjwa unaomsumbua, hupaswa kujua pia aina ya vyakula anavyopaswa kula au kuacha kula, ili kudhibiti tatizo na hatimaye kuliondoa kabisa mwilini.

Leo tunaangalia aina ya vyakula anavyopaswa kula mgonjwa wa Anemia aina zote, ukiwemo Sickle Cell (magonjwa ya kupungukiwa damu mwilini kutokana na sababu mbalimbali).

APPLES
Tufaha au kama linavyojulikana na wengi ‘Apple’ ni tunda muhimu sana kwa wagonjwa wa Anemia. Wanaosumbuliwa na ugonjwa huu, wanashauriwa kula epo 2 hadi 3 kwa kila siku. Tunda hili linaelezwa kusaidia kuongeza kiwango cha madini ya chuma mwilini ambayo huhitajika sana kwenye damu.

VITAMIN B12
Ulaji wa Vitamin B12 ni muhimu sana kwa kinga na tiba ya ugonjwa wa Anemia. Chanzo kikuu cha vitamini hii ni vyakula vitokanavyo na wanyama, hasa nyama ya maini na figo. Nyama hii ni miongoni mwa tiba bora kabisa za ugonjwa huu.
KAHAWA NA CHAI
Hili ndiyo jambo la kuzingatia sana, kwani ndipo ambapo wagonjwa wengi hufanya makosa. Mgonjwa wa Anemia au Siki Seli hatakiwa kunywa chai wala kahawa kwa sababu vinywaji hivi huwa ni kikwazo kwa ufanyaji kazi wa madini ya chuma mwilini.

Unapokuwa mgonjwa wa wa maradhi hayo na ukawa unakunywa chai na kahawa kama kawaida, huwezi kuudhibiti ugonjwa vizuri na dawa utakazokuwa ukitumia hazitafanyakazi ipasavyo, kwa sababu itakuwa ni sawa na mtu anayelala kwenye chandaru kilichotoboka.

BEETS ROOTS
Beets Roots ni aina fulani ya viazi ambavyo vinajulikana pia kama viazi pori. Viazi hivi ni muhimu sana kwa tiba ya ugonjwa wa Anemia kwani vina protini na madini mengi kama vile potassium, phosphorus, calcium, sulphur, iodine, iron, copper, carbohydrates, protein, fat, na vitamin B1, B2, B6, C na P. kwa sababu hii, beets ni tiba nzuri sana ya asili.

MAJI BARIDI
Aidha, uogaji wa maji baridi nao ni sehmu ya tiba asilia ya Anemia. Mgonjwa anashauriwa kuoga maji baridi mara mbili kwa siku. Aidha, uogaji huku ukiwa juani nao husaidia uzalishaji wa Red Cells ambazo ni kiungo muhimu cha damu.

ASALI NA LIMAU
Asali pia imetajwa kuwa tiba nzuri kwa wagonjwa wa Anemia. Changanya asali na limau kiasi kidogo na kunywa asubuhi kabla hujala kitu chochote. Hii nayo ni miongoni mwa tiba bora asilia za ugonjwa huu. Halikadhalika tende zimetajwa kutibu Anemia.

MASSAGE
Ufanyaji wa masaji kila siku nao ni muhimu kwa mgonjwa Anemia, kwani husaidia kuweka juu kiwango cha damu wakati wote. Hii nayo ni moja ya tiba rahisi kabisa unayoweza kuifanya nyumbani kwako.

MWISHO,
Mazoezi mepesi ya kila siku na yale mazoezi ya kuvuta na kushusha pumzi nayo ni muhimu na husadia sana katika kuweka damu katika hali inayotakiwa. Mgonjwa wa Anemia na siko seli akiishi kwa staili ya kufuata maelekezo haya, anaweza asisumbuliwe sana na ugonjwa huo kwa maisha yake yote.

4 comments:

Unknown said...

Okay,asante kwa elimu hiyo

Unknown said...

Upande wa Asali na limao kwa mtoto wa miaka mi 3 inafaa??

Anonymous said...

Ahsante kutujuza

Anonymous said...

Asante sana kwa darasa hilo