Madee vs Afande: Wanakumbusha 2pac na Biggie
Bongo Fleva unapoteza muelekeo, wanamuziki badala ya kujishughulisha kuhakikisha unasimama ili kurudi kwenye chati yake, wenyewe wanakomaa na malumbano.
Huzuni ni kuwa mtu ambaye alionekana ni mr. wisdom kutokana na mashairi yake kubeba ujumbe unaokemea tabia za wanamuziki kulumbana ndiye anayeonekana kushika kasi! Anataka tuamini katika msemo wa kiongozi wa dini feki eti “fuateni maneno yangu, si matendo yangu!”
Suleiman Msindi a.k.a Afande Sele tuna mashaka naye, ndani ya nyimbo zake mbili, Mtazamo na Darubini Kali anakataza malumbano lakini ni yeye huyo huyo leo hii anatupiana madongo na rapa kutoka Manzese, Tip Top Connection, Hamad Ali ‘Madee’.
Ilikuwa ni bifu ya kimya kimya, baadaye Sele akaamua kumchana Madee kwenye wimbo wake Kingdom kuwa janki huyo wa Tip Top ni rais gani anaongea matusi na hana ofisi?
Juzi kati alipohojiwa na kituo kimoja cha redio Bongo, Sele alisema kuwa ni muda mrefu Madee amekuwa akimuimba akaitolea mfano traki, Mikono Juu ambapo alidai kwamba prezidaa huyo wa Manzese alimtusi katika mstari “Umeshawahi kuona wapi Mfalme ana rasta chafu?”
Madee alipoongea nasi, anakana kuwahi kumlenga Afande na kugandamiza kuwa anachojua yeye ni kwamba Mfalme Sele ameishiwa, hivyo anataka kutoka kupitia jina lake. Is it?
Sele alisema: “Bwa’ mdogo Madee ananikubali, unajua yule ni mazao yetu sisi wakongwe ndiyo maana hawezi kuimba bila kunitaja. Mimi mwenyewe namkubali kwa sababu ni mazao yetu yanayofanya vizuri kwenye fani.”
Ni picha mbaya mno, Mfalme Sele ambaye ni mhubiri mzuri wa nyimbo za mipasho, huko nyuma aliwahi kuingia kwenye malumbano na dogo wa Kora Hill Moro, Philipo Nyandindi ‘O Ten’.
Afande na Madee, Wabongo hawapo tayari kusikiliza malumbano yenu kwa sasa, kuna vitu vingi vya kuimba vyenye maana kubwa kwa jamii. Bongo Fleva unaporomoka badala ya kuandika tenzi za kuujengea afya, ninyi mnapigana misumari. Inakera!
Wakali kibao wanaofanya game ya muziki wa Bongo Flava, wameungana na kutoa walichowezeshwa na Muumba Ardhi na Mbingu kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa mafuriko ya Kilosa, Moro.
Mradi wa kuchangia Maafa ya Kilosa kwa wasanii wa Bongo Flava, ulianzishwa na Redio ya Watu Clouds FM na imekuwa ikiwasiliana na mmoja mmoja ili kuhakikisha mastaa wanahusika kwenye matatizo ya jamii.
Tangu Clouds ilipoanzisha harambee hiyo, wasanii wengi wamekuwa wakijitokeza na kutoa kile walichowezeshwa, hivyo kuifanya industry ya muziki Bongo kusogea hatua nyingine kwa wasanii wake kugeuka wahisani kwenye shughuli za kijamii kama ilivyo Mamtoni.
Katika kusindikiza mradi huo wa uchangiaji, mkali wa Hip Hop mwenye vocal za kigumu, Fareed Kubanda ‘Fid Q’ amewahamasisha wenzake na kuingia studio kisha kutoa traki ya maana ambayo hivi sasa inabamba kupitia redio.
Bravo Clouds kwa wazo lenu la maana, pia wasanii na wengine wengi kwa kuitikia wito na kukubali kuvunja benki zenu kwa ajili ya kuwachangia ndugu zetu walioathirika na maafa hayo huko Kilosa, mkoani Morogoro.
Pipi: Mawe 10 tayari, albamu njiani!
Black cutie on Bongo Fleva industry, Doreen Aurelian a.k.a Pipi, yupo tayari kutoka, akiwa na mawe yake 10 mazito anayotaraji kuyajaza kwenye albamu yake ya kwanza ambayo ipo njiani.
Pipi ambaye ni product ya Tanzania House of Talent (THT), amekamilisha mawe hayo ambayo ni strongly katika soko la muziki nchini lakini jina kamili la albamu bado hajapata.
“Albamu tayari lakini jina bado, nipo natafakari pamoja na menejimenti yangu kuhusu wimbo utakaonza kuchezwa hewani ili kuitangaza albamu yangu,” alisema Pipi ambaye alichomoza kupitia traki ya Njiapanda ambayo ni mali ya Barnabas na kuongeza:
“Inawezekana nikarelease Usinune ambao nimefanya na Barnabas au Bora Wewe ambao nimekomaa nao mwenyewe.”
Aliongeza, mzigo mzima umesimamiwa na THT na nyimbo zimerekodiwa Bongo Record kwa Majani, 59 Records, B Hits Company kwa Hermy B na Duke.
Alitaja nyimbo nyingine na wasanii aliowashirikisha kuwa ni Moyo ft G. Nako & Juacali, Ukiniacha, Usikatae, Bora Wewe, Nilikupenda, Njiapanda (amekubaliana kushea na Barnabas) na Usinune.
Nyota Ndogo Ageukia muziki wa Injili
Mkali wa muziki wa kizazi kipya Afrika Mashariki, Nyota Hassan Ndogo amefanya ‘wandaz’ na hivi sasa kule pande za Kenya ni gumzo baada ya kuingiza vocal kwenye wimbo mmoja wa Injili.
Inajulikana kwamba Nyota ni Muislamu, kitendo chake cha kuimba Injili kimechukuliwa kama anaisaliti imani yake, hivyo kuibua mjadala mkubwa nchini Kenya hususan Mombasa.
Katika wimbo huo, Nyota ameshirikishwa na mwimbaji wa Injili, Gabriel.
Hata hivyo, Nyota amesema kwamba yeye ni Mwislamu kamili na imani yake haijatetereka isipokuwa aliingiza vocal kwenye wimbo huo kwa sababu aliombwa na mwenzake kufanya hivyo kisanii.
Megan Fox: Asaliti, ampa penzi Cristiano Ronaldo
Abby Cool & MC George over the weekend bado ipo kazini na Ebwana Dah! Ndiyo jina la column yetu. Kama kawa ikiachana na mmoja, wiki inayofuata inahusika na mwingine katika mtindo bora zaidi.
Muigizaji Megan Fox ndiye staa anayepanda kizimbani leo na hapa inatajwa orodha ya wanaume ambao kwa nyakati tofauti, kwa ridhaa yake na mapenzi tele aliamua kujipurua mavazi mwilini na kuwapa penzi lake.
Kwa mujibu wa ‘site’ ya intaneti inayojihusisha zaidi na habari za uhusiano wa mastaa katika eneo la nani kamrukia nani, wanaume ambao wanatajwa kuwahi kufaidi penzi la Megan ni wanne!
Kubwa linalochukua nafasi kwenye ishu ya Megan ni staa huyo kumsaliti mpenzi wake Brian Austin Green na kumpa penzi mwanasoka wa kimataifa wa Ureno, anayekipiga Klabu ya Real Madrid ya Hispania, Cristiano Ronaldo.
Inaelezwa kuwa wakati Megan akiwa na sweetheart wake Brian, alikolea kwa Ronaldo, hivyo bila hiyana akaamua kukwea naye on bed na kujikunja kisela kwa mahaba motomoto.
Hata hivyo, inawekwa wazi kuwa pamoja na Megan kumpa penzi Ronaldo lakini Brian alichukulia poa, hivyo mpaka leo bado wapo pamoja na yote yanayohusu mapenzi wanayanogesha kama kawa!
Katika listi ya wanaume wa Megan, anayetajwa wa kwanza kuchangamka naye ni Ben Leahy aliyechetuana naye kati ya mwaka 2000 – 03, akaja David Gallagher mwaka 2003 – 04, mwaka 2005 akahamishia majeshi kwa Brian ambaye kinaeleweka mpaka leo. Mwaka 2009 ndiyo alimuonjesha Ronaldo.
Jina lake kamili ni Megan Denise Fox, alizaliwa Mei 16, 1986, Rockwood, Tennessee, Marekani. Ni mhitimu wa St. Lucie West Centennial High School, Port St. Lucie, Florida, Marekani na muvi iliyomtoa ni Transformers.

************************************
Wakali Bongo Flava wanyoosha mikono MAAFA KILOSAWakali kibao wanaofanya game ya muziki wa Bongo Flava, wameungana na kutoa walichowezeshwa na Muumba Ardhi na Mbingu kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa mafuriko ya Kilosa, Moro.
Mradi wa kuchangia Maafa ya Kilosa kwa wasanii wa Bongo Flava, ulianzishwa na Redio ya Watu Clouds FM na imekuwa ikiwasiliana na mmoja mmoja ili kuhakikisha mastaa wanahusika kwenye matatizo ya jamii.
Tangu Clouds ilipoanzisha harambee hiyo, wasanii wengi wamekuwa wakijitokeza na kutoa kile walichowezeshwa, hivyo kuifanya industry ya muziki Bongo kusogea hatua nyingine kwa wasanii wake kugeuka wahisani kwenye shughuli za kijamii kama ilivyo Mamtoni.
Katika kusindikiza mradi huo wa uchangiaji, mkali wa Hip Hop mwenye vocal za kigumu, Fareed Kubanda ‘Fid Q’ amewahamasisha wenzake na kuingia studio kisha kutoa traki ya maana ambayo hivi sasa inabamba kupitia redio.
Bravo Clouds kwa wazo lenu la maana, pia wasanii na wengine wengi kwa kuitikia wito na kukubali kuvunja benki zenu kwa ajili ya kuwachangia ndugu zetu walioathirika na maafa hayo huko Kilosa, mkoani Morogoro.
*******************
Pipi: Mawe 10 tayari, albamu njiani!
Black cutie on Bongo Fleva industry, Doreen Aurelian a.k.a Pipi, yupo tayari kutoka, akiwa na mawe yake 10 mazito anayotaraji kuyajaza kwenye albamu yake ya kwanza ambayo ipo njiani.
Pipi ambaye ni product ya Tanzania House of Talent (THT), amekamilisha mawe hayo ambayo ni strongly katika soko la muziki nchini lakini jina kamili la albamu bado hajapata.
“Albamu tayari lakini jina bado, nipo natafakari pamoja na menejimenti yangu kuhusu wimbo utakaonza kuchezwa hewani ili kuitangaza albamu yangu,” alisema Pipi ambaye alichomoza kupitia traki ya Njiapanda ambayo ni mali ya Barnabas na kuongeza:
“Inawezekana nikarelease Usinune ambao nimefanya na Barnabas au Bora Wewe ambao nimekomaa nao mwenyewe.”
Aliongeza, mzigo mzima umesimamiwa na THT na nyimbo zimerekodiwa Bongo Record kwa Majani, 59 Records, B Hits Company kwa Hermy B na Duke.
Alitaja nyimbo nyingine na wasanii aliowashirikisha kuwa ni Moyo ft G. Nako & Juacali, Ukiniacha, Usikatae, Bora Wewe, Nilikupenda, Njiapanda (amekubaliana kushea na Barnabas) na Usinune.
******************
Nyota Ndogo Ageukia muziki wa Injili
Mkali wa muziki wa kizazi kipya Afrika Mashariki, Nyota Hassan Ndogo amefanya ‘wandaz’ na hivi sasa kule pande za Kenya ni gumzo baada ya kuingiza vocal kwenye wimbo mmoja wa Injili.
Inajulikana kwamba Nyota ni Muislamu, kitendo chake cha kuimba Injili kimechukuliwa kama anaisaliti imani yake, hivyo kuibua mjadala mkubwa nchini Kenya hususan Mombasa.
Katika wimbo huo, Nyota ameshirikishwa na mwimbaji wa Injili, Gabriel.
Hata hivyo, Nyota amesema kwamba yeye ni Mwislamu kamili na imani yake haijatetereka isipokuwa aliingiza vocal kwenye wimbo huo kwa sababu aliombwa na mwenzake kufanya hivyo kisanii.
***********************
Megan Fox: Asaliti, ampa penzi Cristiano Ronaldo
Abby Cool & MC George over the weekend bado ipo kazini na Ebwana Dah! Ndiyo jina la column yetu. Kama kawa ikiachana na mmoja, wiki inayofuata inahusika na mwingine katika mtindo bora zaidi.
Muigizaji Megan Fox ndiye staa anayepanda kizimbani leo na hapa inatajwa orodha ya wanaume ambao kwa nyakati tofauti, kwa ridhaa yake na mapenzi tele aliamua kujipurua mavazi mwilini na kuwapa penzi lake.
Kwa mujibu wa ‘site’ ya intaneti inayojihusisha zaidi na habari za uhusiano wa mastaa katika eneo la nani kamrukia nani, wanaume ambao wanatajwa kuwahi kufaidi penzi la Megan ni wanne!
Kubwa linalochukua nafasi kwenye ishu ya Megan ni staa huyo kumsaliti mpenzi wake Brian Austin Green na kumpa penzi mwanasoka wa kimataifa wa Ureno, anayekipiga Klabu ya Real Madrid ya Hispania, Cristiano Ronaldo.
Inaelezwa kuwa wakati Megan akiwa na sweetheart wake Brian, alikolea kwa Ronaldo, hivyo bila hiyana akaamua kukwea naye on bed na kujikunja kisela kwa mahaba motomoto.
Hata hivyo, inawekwa wazi kuwa pamoja na Megan kumpa penzi Ronaldo lakini Brian alichukulia poa, hivyo mpaka leo bado wapo pamoja na yote yanayohusu mapenzi wanayanogesha kama kawa!
Katika listi ya wanaume wa Megan, anayetajwa wa kwanza kuchangamka naye ni Ben Leahy aliyechetuana naye kati ya mwaka 2000 – 03, akaja David Gallagher mwaka 2003 – 04, mwaka 2005 akahamishia majeshi kwa Brian ambaye kinaeleweka mpaka leo. Mwaka 2009 ndiyo alimuonjesha Ronaldo.
Jina lake kamili ni Megan Denise Fox, alizaliwa Mei 16, 1986, Rockwood, Tennessee, Marekani. Ni mhitimu wa St. Lucie West Centennial High School, Port St. Lucie, Florida, Marekani na muvi iliyomtoa ni Transformers.
********************
compiled by mc george
1 comment:
Naomba niulize swali kuhusiana na Hassan Ndogo kuimba wimbo wa Injili. Hivi waisilamu hawaruhusiwi kujiamulia maisha yao wenyewe bila kuamuliwa kila jambo na waisilamu wote? Kwani Muisilamu akiamua kubadili dini kuna ubaya gani? Nionavyo mimi waisilamu ni kama wako Jela. Hawana uhuru wa kujiamulia mwelekeo wa maisha? Sisi wa dini zingine unaweza ukabadili dini yako wakati wowote kwani ni maisha yako siyo ya umma.
Post a Comment