Friday, March 5, 2010

IJUMAA SHOWBIZ!

BELINA “Bongo hakuna ishu, nasepa”
Modo ‘the big name’ Bongo, Belina Mgeni yuko so tired na tenda za modeling hapa home, anadai katika industry hiyo hakuna dili zaidi ya kutaabika kiaina.

Akisema na ShowBiz jijini Dar es Salaam mwanzoni mwa wiki hii, Belina alidai kuwa yuko mbioni kusaka Modeling Company za Sauzi ambako anaamini fani hiyo inalipa hata kama kuna msoto kiasi fulani.

“Sanaa ya mitindo Bongo hailipi, sijui tunakosea wapi, lakini nadhani watu bado hawajaamka kama kwa wenzetu, bora nikatafute dili Sauzi, najua huko wako mbele zaidi,” alisema Belina ambaye ni mama wa mtoto mmoja.
***************************************************

Joyce Kiria :uso kwa uso na Vicky Kamata

Presenta wa Bongo Movies kunako stesheni ya Runinga ya East Africa ‘EATV’,Joyce Kiria Nkongo, kesho anatarajia kuwapasha habari njema wanawake kwenye program yake inayokwenda kwa jina la Wanawake Live.

Kiria alisema na Showbiz wiki hii kwamba, ishu hiyo itachukua nafasi ndani ya Ukumbi wa DICC uliopo Posta, Dar es Salaam ambapo mwanamuziki ‘mwanampotevu’, Vicky Kamata atakuwepo kwa ajili ya kutoa sapoti zaidi.

Stelingi alisema kipindi hicho kitakachoanza saa 7:00 mchana ni spesho kwa kwa ajili ya kuwapa wanawake mwamko wa kimaisha na uchumi ambapo kutakuwa ma ladies waliofanikiwa kimaisha ambao watatoa hamasa kwa wengine.
*****************************************

Luiza na mwanae

Luiza Mbutu: Hii ya mwanaye kali

Blood son wa mwanamuziki mkongwe from Bendi ya dansi, African Stars ‘Twanga Pepeta International’, Luiza Mbutu, Brayan Mbutu, ametoa kali baada ya kuambiwa ataletewa mdogo wake na kuanza kuangua kilio, Kyala Seheye alikuwepo eneo la tukio.

Ishu hiyo ilitake place nyumbani kwao pande za Mwananyamala, jijini Dar juzikati, wakati mama yake akiendelea kuangusha story na safu hii, ghafla Brayan aliibuka na kuanza kufanya fujo.

Katika kumtuliza, Mbutu alimwambia endapo ataendelea kufanya vurugu mbele ya macho ya ShowBiz atalazimika kumletea mdogo wake. Kusikia ishu hiyo, Brayan alizidisha kilio huku akimuomba mama yake please asimletee mdogo wake.

Safu hii ilimtight Brayan kwanini hataki kuletewa mdogo wake ambapo alisema: “Akija mdogo wangu, mama atakuwa hanipendi tena.”
*****************************************************

FID Q Amgongesha Bi. Kidude Hip Hop
Staa mwenye heshima kubwa kunako anga ya muziki wa kizazi kipya, Fareed Kubanda ‘Fid Q’, ndani ya albamu yake yenye lebo ya Propaganda itakayodondoka kitaani Jumatatu ijayo kuna jiwe alilogonga kolabo na mkongwe wa miondoko ya mwambao, Fatuma Baraka ‘Bi. Kidude.

Akipiga stori na ShowBiz, Dar es Salaam juzi, mkali huyo wa ngoma ya Usinikubali haraka alisema kuwa kazi aliyofanya na Bi. Kidude inakwenda kwa jina la Juhudi za wasiojiweza ambayo ni Hip Hop iliyotengenezwa katika environment ya Visiwa vya Zanzibar.

“Ngoma nyingine zitakazokuwa ndani ya Propaganda yenye nyimbo 12 na vichwa nilivyovishirikisha ni pamoja na Hey Lord (Mzungu Kichaa), Temanoleji, Wananiita King (Nylon wa Manzese Crew), Mama (Bizman), Ripoti za Mtaa (Zahir Zorro), Kila Siku (Q-Jay), Shimo limetema (Ncha Kali na AY), na nyingine,” alisema.
******************************************


Kala

R O M A


R.O.M.A & KALA: Kukutana ‘Peponi’

Ishu mpya ilidondoka pande hizi za ShowBiz katikati ya wiki hii inachana kuwa vichwa viwili vinavyofanya poa katika game ya muziki wa Hipo Hop, Ibrahim Musa a.k.a R.O.M.A’ na Kala Jeremiah vipo kunako mishemishe za kuangusha kolabo ya ajabu yenye idea ambayo itawakutanisha ‘peponi’ kimawazo.

Ndani ya safu hii R.O.M.A alisema ngoma hiyo wanaifanya kwenye Studio ya Tongwe Reords ambapo yeye ataekti kama ni mmoja wa viongozi waliotangulia mbele ya haki siku nyingi na Kala atachukua position ya kiongozi aliyefariki dunia hivi karibuni kisha wanakutana huko na kujadiliana mambo mbalimbali kuhusu nchi yao.

“Wakati bado kazi zangu, Tanzania na Mr. President zikiendelea kushaini hewani soon natarajia kuachia ngoma nyingine yenye jina la Patric Kamugisha iliyogongwa Tongwe Records chini ya prodyuza J. Murder, nimeamua kufanya idea tofauti baada ya kuhisi nyimbo za siasa zinaniletea matatizo kimtindo, lakini siyo kwamba nimeacha kufanya kabisa, nitaendelea kuwakosoa viongozi, isipokuwa hivi sasa napumzika kwa muda,” alisema R.O.M.A.

Compiled by mc george/ijumaa showbiz

No comments: