Madee & Pendo: Sote tudondoshe chozi
Siku zinakatika na binadamu wanazaliwa wengine wanaiacha dunia kwa staili tofauti. Mungu ni sababu ya kila kitu lakini ni maumivu yasiyo na mfano kumpoteza mtu unayempenda.
Staa wa Bongo Fleva, Hamad Ali ‘Madee’ (pichani juu, enzi za penzi motomoto) yupo kwenye kipindi kigumu zaidi, wiki iliyopita alimpoteza mchumba wake, Pendo. Kwa wadau wa muziki, jina la Pendo lipo ‘live’ masikioni kwa sababu ameimbwa sana na wasanii. Pendo alifariki dunia kwa ajli ya gari iliyotokea kwenye Kijiji cha Ubena, Pwani baada ya basi alilokuwa amepada, Shabiby kugongana na lori.
Ni wazi kwamba maumivu ya Madee na familia ya Pendo hayapimiki lakini ni vema kukumbuka kuwa sote ni wa Mwenyezi Mungu na kwake kila nafsi itarejea. Abby Cool & MC George over the weekend tunatoa pole kwa Madee na familia ya Pendo. Mashairi ya wimbo wa Madee ‘Kazi yake Mola’ yana maana kubwa, tuyatafakari.
Mwili wa marehemu Pendo unatarajiwa kuagwa leo katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili kabla ya kus afirishwa kwenda Moshi kwa mazishi.
H. Mbizo naye ajitosa kwenye taarabu
Dogo aliyewahi kusimama vema kwenye ulingo wa Bongo Fleva, Hassan ‘H’ Mbizo, naye ameamua kujitosa kwenye Taarab baada ya ‘kuskuti’ na kuona things are not easy.
H. Mbizo aliyewahi kutamba na nyimbo kama Mchumba na Nilonge Nisilonge, hivi sasa yupo Studio ya Poteza Records, iliyopo Temeke akipika jiwe la Taarab. Hii ipo confirmed na baada ya H. Mbizo haijulikani nani atafuata. Wakali wengine wa Bongo Fleva ambao wamevamia Taarab ni Babu Ayoub, Aboubakar Mzur, Q Chillah, Hammer Q na wengine wachache.

*********************************

****************************
Bongo Flava: Eti uchawi una nguvu kuliko vipaji!
Yupo mwanafilosofia aliyewahi kutamka kwamba desturi ya mvivu ni kutokujiamini, pale anapoonekana anaanza kushindwa huanza kutafuta mchawi.
Kutokana na falsafa hiyo, inawezekana uswahilini wavivu ni wengi kwa sababu ndiko kwenye idadi kubwa ya watu wanaowashika wenzao uchawi. Majirani hawaelewani! Waganga wanawachonganisha!
Desturi hiyo imetua Bongo Fleva, some artists wameanza kurusha maneno kwenda kwa wenzao. Wanalaumu kwamba wanarogwa ndiyo maana hawapigi hatua na chati yao imeshuka. Is It? Wizi mtupu! Let us agree with that philosopher, huu ni uvivu.
Wasanii hawaumizi vichwa kuleta tungo bora, badala yake wanawaza mambo mepesi ambayo hayauziki, wakiangukia pua sokoni wanadai wamerogwa. Wewe nani mpaka uhisi unarogwa? Ni wazi kwamba kauli za ‘mamentali’ wanaolalamika kurogwa, zina maana ya kuwa uchawi una nguvu kuliko vipaji. Yaani Mungu aliyetoa zawadi ya asili kwa mja wake, inaweza isifanye lolote ikiwa kiumbe mwingine ataamua kuichezea gizani.
Si kweli! Mungu si wa rahisi kwa kiwango hicho, na katika hili wasanii wanatakiwa kuachana na uvivu wa kufikiri. Wafanye kazi kwanza halafu matunda wayaone, si kubweteka, kulewa sifa mjini halafu wanapoporomoka, waanze kulaumu wengine.
Hakuna mchawi mbele ya Mungu, kama wachawi wangekuwa na nguvu pengine leo hii kusingekuwa na mabilionea. Wangerogwa kisha wangepiga mweleka kila mara ambapo wangejitahidi kuchomoza. Mbona wangine wanafanikiwa? Ya nini ukose amani kwa kutafuta mambo ambayo mwisho wa siku yatakupoteza? Ni vema kutafakari kwa kichwa kuliko kuamini macho na masikio.
Usher:Staili 10 za kubadili warembo kitandani, aibuka na demu mpya
Nidhamu ya Ebwana Dah! Ni kuhakikisha kila Jumatatu inakupa kitu murua kuhusu mastaa wa kiwanja katika eneo la nani katoka wapi kamrukia nani, huo ndiyo mpango mzima.
Ni Usher Raymond na staili zake za kubadili totoz, mtandao unaodili na ishuz za mastaa wa kiwanja, unaanika majina ya wanyange 10 ambao kwa nyakati tofauti, staa huyo wa R&B ameweza kukwea nao on bed.
Kwa mujibu wa mtandao huo, mrembo Ayesha Butler ndiye anatajwa wa kwanza lakini haiwekwi wazi ni lini walichetuka kama ilivyo kwa Karrine Steffans. Mwaka 1995, Usher alifanya kweli na Monica, pia akaunga staili ya mtu na rafiki yake, alipotoka na Brandy Norwood kuanzia mwaka 1998 na kutemana 1999.
Wadaku wanadai kuwa baada ya Usher kuchetuka na Monica kisha Brandy, ndipo warembo hao walipoamua kutoka na wimbo, The is Mine. Mwaka 2001 – 04 kilikuwa ni kipindi kizuri kwa Usher na staa wa TLC, Rozonda Chilli Thomas na kufikia kutangaza ndoa, lakini kwa utukutu wake wa kucheza ‘nje kapu’, mwaka 2002 alidondoka dhambini na Melinda Santiago.
Mwaka 2004, Usher alinasa kwenye penzi la Naomi Campbell, mwaka 2005 akajichuja na Joy Bryant, mwaka huo huo Eishia Brightwell, pia mwaka 2005 – 09, alijituliza kwa Tameka Foster.
Kwa sasa, Usher yupo na kimwana Grace Miguel na uhusiano wao ulianza tangu mwaka 2009. Alizaliwa Oktoba 14, 1978, Atlanta, Georgia, Marekani, umri wake ni miaka 31.
Mlela kutoka na muvi yake
The Ijumaa Sexiest Bachelor 2009 - 2010, Yusuf Mlela atakuwa sawa kutoka na muvi moja kali ambayo inatokana na mradi wake binafsi ifikapo Aprili 2010. Mlela, alisema nasi last week kwamba muvi hiyo itasimama kwa jina la Black and White na itawashirikisha mastaa kadhaa Bongo. “Filamu yangu itasimama vizuri, stori nzuri pia wasanii watakaocheza ni wakali, mimi mwenyewe ndani,” alisema Mlela ambaye hujisikia raha akifananishwa na Angelo wa The Promise.
compiled by mc george/Ijumaa Wikienda

********************************************

***************************************
Mlela kutoka na muvi yake
The Ijumaa Sexiest Bachelor 2009 - 2010, Yusuf Mlela atakuwa sawa kutoka na muvi moja kali ambayo inatokana na mradi wake binafsi ifikapo Aprili 2010. Mlela, alisema nasi last week kwamba muvi hiyo itasimama kwa jina la Black and White na itawashirikisha mastaa kadhaa Bongo. “Filamu yangu itasimama vizuri, stori nzuri pia wasanii watakaocheza ni wakali, mimi mwenyewe ndani,” alisema Mlela ambaye hujisikia raha akifananishwa na Angelo wa The Promise.
compiled by mc george/Ijumaa Wikienda
No comments:
Post a Comment