Umeona shavu la Tonya?
Ule usemi kuwa, duniani hakuna mtu mwembamba umeleta maana baada ya ShowBiz kumbamba live staa wa Bongo Flava, Seif Shaban ‘Matonya’au Tonya akiwa shavu dodo (mcheki pichani) tofauti na alivyokuwa siku kadhaa zilizopita.
Truly, Tonya aliyebambwa ndani ya Ukumbi wa Paradise City Hotel , Dar es salaam akiwa kwenye Mkutano wa Waandaji wa Tanzania Music Awards na wasanii mwanzoni mwa wiki hii anaonekana kuridhika kwani amekuwa bonge la mtu ‘more power’, hivyo kuibua idea kuwa yawezekana staa huyo wa ‘Teksi Bubu’ anapata kitu roho inataka kutoka kwa 'mai waifu' wake tofauti na ilivyokuwa before marriage.
ShowBiz inatumia chance hii kumshauri mchizi kupiga tizi in order kujiweka safi ili asishindwe kufanya kweli kunako steji kwani wapo baadhi ya wasanii wamejiachia na inapotokea wakapata shoo jukwaani huchukua dakika chache na kuanza kuhema kama wanakimbizwa! Umeona?!!!
***********************************************************
******************************************************************
Kauli za wasii kuhusu TANZANIA MUSIC AWARD 2010
Kutoka pande za Posta Mpya, Dar es Salaam mwanzoni mwa wiki hii Waandaaji wa Tuzo za Muziki Tanzania walikutana uso kwa uso na baadhi ya mastaa wanaofanya vyema kunako game hiyo ndani ya Ukumbi wa Paradise City Hotel, uliopo kwenye Jengo la Benjamini Mkapa.
Ishu kubwa ilikiwa ni kubadilishana mawazo kwa ajili ya kuziboresha zaidi sherehe hizo ambazo kwa miaka kibao zilionekana kuwa na dosari za hapa na pale.
Wasanii kadhaa walipata nafasi ya kuongea kile kilichomo mioyoni mwao ili waandaaji hao wakakifanyie kazi. Soma kauli zao hapo kulia kuanzia na Jide:
JIDE: "Kwasababu tuzo hizi ni za Kitaifa ingekuwa vizuri kama zingepewa jina la Kiswahili kama “Tuzo za Muziki wa Tanzania” badala ya Tanzania Music Awards ili hata wananchi waishio Mtwara, Tarime na kwingine nchini wawe wanazifahamu kwa urahisi zaidi.”
AY: "Mimi nashauri kwamba, badala ya kuwapa washindi zawadi mbalimbali ikiwemo pesa na kuwaacha ni vyema waandaaji wakafikiria kuwapa mikataba ya kufanya matangazo ya kampuni yao kwa kipindi cha mwaka mmoja wa ushindi wao ikiwemo kufanya shoo mbalimbali watakazoandaa.”
Wakati huo huo: FA A.Y ndiyo meneja wangu
Ishu mpya iliyodondoka pande hizi inawahusu mastaa wawili wenye majina in the Bongo Flava, Khamis Mwinjuma ‘FA’ na Ambwene Yesaya ‘A.Y’, wako hand in hand katika kusukuma gurudumu la maisha.
Akipiga story na ShowBiz Dar juzikati, FA alitoa bonge la surprise pale alipoweka plain kwamba, kwa sasa meneja wake ni A.Y ambaye yuko mbioni kumaliza masomo yake ya biashara yaliyokuwa yakimuweka tight.
Akiwa na three weeks only tangu arejee Bongoland from kiwanja, mtu mzima FA alisema na safu hii kuwa mapema next week ataanza project mpya na meneja wake ambayo wataipa title hapo baadaye.
“Project hiyo itafanyika ndani ya B-Hits Company chini ya maprodyuza Hermy B na Pancho,” alisema.
****************************************************
WITNESS: "mna uwezo mkubwa wa kutulipa vizuri, bora mngekuwa mnatulipa vizuri badala ya kuwaleta wasanii kutoka nje ambao hawaji bila kuwalipa dola laki tatu..!"
***************************************************
Bebe cool: Full kujiachia na Zuwena tenaFew days baada ya Artist mwenye heshima kubwa kutoka pande za Museveni nchini Uganda, Bebe Cool kushambuliwa kwa risasi na Polisi, amerejea kwenye form kwa kasi na kuachia ngoma mpya yenye jina la Kasepiki ikiwa na video yake huku mkewe , Zuena ambaye walitengana mwishoni mwa last year akionekana kuwa karibu naye zaidi.
ShowBiz imeperuzi na kudadisi kisha kuibuka na story kwamba, lovers hao walianza kuwa close baada ya Bebe kupigwa risasi. Full story ni kwamba Zuwena ni tekniko woman kwani baada ya kupata nyiuzi kwamba jamaa ana hali mbaya, alimua kutumia muda wake mwingi kumfariji hadi wakafanikiwa kuwa pamoja tena huku wakipuuzia maneno ya mahasimu wake wakiwemo Weasal na Redio.
compiled by mc george/Ijumaa Newspaper
No comments:
Post a Comment