Thursday, April 1, 2010

IJUMAA SHOWBIZ!

 JB Mpiana:>>Mwaka huu mgumu kwa wakongwe
This is soon after kuchemsha sokoni kwa albam yake iliyopita, Prezidaa wa Crew ya Wenge Musica (BCBG) inayotamba kunako Flava za Soukouss  huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Jean Bedel Mpiana ‘JB Mpiana’, ametoa sound na kusema: “Mwaka huu ni mgumu kwa wakongwe kwani chipukizi wanaochipukia wanafunika ile mbaya!” 
 
Mpiana a.k.a Suviere Premiere  Binadamu, aliyasema hayo alipokuwa akistorisha na mtandao mmoja wa burudani nchini humo  na kuweka plain kwamba, yuko kwenye process ya kuachia albam mpya aliyoipa jina la  ‘Aller Soyons Serieux’ (tuwe makini),  hii ikiwa ni few days baada ya kufanya onyesho  spesho lililokuwa linakwenda kwa jina la St. Valentine 2010.
 
 “Ni vigumu kuamini kuwa wanamuziki wa kizazi cha sasa cha Soukouss, Fally Ipupa, Ferre Gola, Soleil Wanga, Shikito na wengine wamefanikiwa kupiga hatua kubwa katika muziki na kujikuta wanawafunika wakongwe,” alisema Mpiana.
         ***************************************
 xxl Teen music awards 2010: Ni kifo kundi bora
Katika hali isiyokuwa normal, hivi sasa mchakato wa kutafuta washindi katika tuzo za heshima, XXL  Teen Xtra Award 2010, unazidi kushika kasi huku  kinyang’anyiro cha kutafuta kundi bora la mwaka kikionekana kuwa-mix  ile mbaya fansi wa music wa Bongo kutokana na ukali wa makundi yaliyopangwa in that kategori.
 
Kwa mujibu wa data zilizokusanywa kutoka  Mtandao wa Nipe5.com, mashabiki wengi wa muziki wa Bongo wanaonekana  kubaki na sintofahamu huku pia wakiwa na hamu kubwa ya kutaka kujua ni kundi gani litafunika  na kutwaa tuzo hiyo  kati ya sita yaliyopo, yakiwemo ‘Wakali kwanza (H1), Wateule (H2), Nako 2 Nako (H3), Offside Trick (H4) Tip Top Connection  (H5) na TMK Wanaume (H6).
 
Kinyang’anyiro hiki kinatarajiwa kumalizika mwishoni mwa mwezi huu  ambapo winners watapatikana kupitia kura zinazopigwa na mashabiki hivi sasa kupitia mtandao wa Nipe5.com ama kwa  njia ya simu kwa kuandika jina la kundi na namba ya ushiriki kama unavyoziona hapo juu kisha kutuma kwenda namba 15551.
**********************************************
 

Lord Eyez: Ahurumiwa, atakiwa kurudi nyumbani kwao A-Town

Kutoka pande za A-town, ShowBiz ina-break silence ya baadhi ya wasanii wa filamu wa pande hizo kwamba wanamhurumia ile mbaya nyota wa Nako 2 Nako, Isaack Waziri Makuto a.k.a  ‘Lord Eyez’ wakimtaka arudi nyumbani kuendeleza libeneke huenda afya yake itakuwa poa.

Jamaa hao wa Crew ya Maigizo ya Serious Actors & Actress, walitoa saunds zao kwa pamoja mbele ya safu hii walipokuwa kwenye tour jijini Dar juzikati ambapo walisema tangu jamaa atimke Arusha na kuwa in love na Bongo Music Diva, Rehema Chalamila ‘Ray C’, everything about music kiko upside down kwa upande wake.

“Ebwana, Lord Eyez amepungua ile mbaya, anatia huruma so ni bora arejee kitaani Arusha tuendeleze ladha za machalii katika Bongo Flava, huenda pia afya yake ikarudi kama zamani,” alisema mmoja wa ma-artists hao.
                     *********************************************************

Trina:>> ‘Million Dollar Girl’ yamuweka ‘Another Level’ 
It is another time Ladies and gentlemen, mwanadada mwenye makeke ya ‘kumwaga’ kunako game ya Hip Hop kutoka mambele (Marekani), Katrina Laverne Taylor ‘Trina’, amekwea juu ya kilele cha mafanikio baada ya  kukamilisha mpango mzima wa video ya ngoma yake ya ‘A Million Dollar Girl’ iliyowafunga midomo wapinzani wake. 
 
Kwa mujibu wa stori kutoka ‘LAT’, video ya ngoma hiyo imetengenezwa na mkali, Nicki Minaj na ni mzigo namba moja katika albamu yake ya New brand iliyopachikwa jina la ‘Amazin’.
******************************************
compiled by mc george/ijumaa newspaper

No comments: