Lil` Weezy ambaye kwa sasa yupo jela akitumikia kifungo cha mwaka mmoja jela baada ya kubanwa na shtaka la kukutwa na silaha ya moto kinyume cha sheria, jicho letu ‘tovutini’ limebaini kwamba amewahi kutoka kimahaba na wadada sita.
Site ya kishambenga iliyopo US ambayo ime-specialize katika kufuatilia issues za uhusiano wa kimapenzi na mastaa wa Kiwanja, inafunua kuwa Weezy, alianza mapenzi akiwa na umri wa miaka 13.
Antonia Carter ndiye anayetajwa wa kwanza, huyo alidondoka naye dhambini kuanzia mwaka 1996 – 06, lakini akiwa naye, kati ya mwaka 2003-05, dogo huyo ‘alisuuzana’ kisela na sistaduu, Christina Milian.
Kati ya mwaka 2003-09, Weezy pia akajiweka kwa Nivea na 2005-06, alikwenda sawa na demu mgumu, Trina, 2005-08, akafanya kweli na Sarah Bellew na kuanzia 2007 hadi mwaka huu, penzi la tuff wallet huyo wa Cash Money, lilidondoka kwa Lauren London.
Hata hivyo, site hiyo inamchambua Lauren kwamba kabla ya ‘kusugua’ na Weezy, alikuwa na Baron Davis na Chris Foxx ambaye alichangamka naye mwaka 2006.
Jina lake kamili ni Dwayne Michael Carter Jr, alizaliwa Septemba 27, 1982, New Orleans, Louisiana, Marekani. Umri wa miaka 27, dini yake ni Mkristo.
Hasheem Vs Top in Dar
Majibizano yao katika jokes!
Inavuma kitaani, kila mmoja anajaribu kusema lake kuhusiana na ugomvi wa mastaa wawili, staa wa NBA anayekipiga kwenye Klabu ya Memphis Grizzlies, Hasheem Thabeet na icon wa Bongo Fleva, Khaleed Mohamed ‘TID’.
Mengi yamezungumzwa lakini ipo ishu ya utani ambayo inatajwa. Kuanzia walipoonana, wakaanza kujibizana na baadaye kipigo. Usisahau ishu ya yule dogo aliyekula mbata a.k.a kerbu kutoka kwa staa huyo wa NBA.
Eti ishu ilianza hivi;
TID na chombo chake, walikuwa wanakula mema ya nchi ndani ya Club Bilicanas, Dar muda fulani hivi baadaye, Hasheem akatokea, huku akiwa ameongozana na washkaji kadhaa.
Eti, demu wa TID alipomuona Hasheem akapagawa, “wooow”, hiyo Top In Dar ikamuudhi, akaweka bifu.
Akangoja Hasheem apite, akamuanzishia kama hivi;
TID: Oyaa, we’ dogo unajiona umemaliza kila kitu?
Hasheem: Kivipi bro?
TID: Unajua dogo unajiona matawi sana?
Hasheem: Sijakuelewa kaka.
TID: Mbona unapita bila kusalimia?
Hasheem: Ooh, nikupitiwa you know, samahani.
TID: You know nini? Shauri yako!
Hasheem: Nimekuomba msamaha.
TID: Msamaha wapi? Yaani sisi tushindwe kutanua na mademu zetu kisa wewe?
Hasheem: Mbona sikuelewi?
TID: Ntakufanyia kitu mbaya!
Hasheem: Huko unakokwenda siyo kabisa.
TID: Mi’ mtoto wa Kino, nitakuharibia halafu tutakomba vyote vya mwilini.
Hasheem: Basi kama vipi jaribu.
TID: Alafu wewe unajidaia urefu wako.
Hasheem: Oyaa, nitaku-dunk kama basketball?
TID: Jaribu, mimi nitakubutua kama football au nitakukumbatia kama MIC.
Hasheem: Maneno mengi ya nini? Jaribu!
TID: Unajidai una pesa, mimi nimekuwa staa wa nchi hii kabla yako.
Hasheem: Naona hauna la kuongea, naondoka!
TID: Oyaa, mbona unaondoka, hatupigani tena?
Eti baada ya hapo, jamaa akamchota mtama mmoja ambao ulikaribia kuondoa uhai wa mtu. Ila hii siyo hali halisi iliyotokea, its only jokes.
Kuhusu brothermen aliyekula kibao;
Brothermen: Duh, huyu jamaa mrefu!
Hasheem: Ndiyo kaka, mimi mrefu, unasemaje?
Brothermen: Aah, kwani nini?
Hasheem: Anyway, poa.
Brothermen: Poa nini? Naona siku hizi unajidaia vogue lako.
Hasheem: Duh!
Brothermen: Halafu sisi kitaani hatukufagilii wala nini?
Hasheem: Naomba tuheshimiane basi!
Brothermen: Akuheshimu nani? Unafikiri mimi TID, nitakupa kipondo?
Hasheem: Unaweza kunipiga?
Brothermen: Yap, sogea hapa uone.
Baada ya hapo jamaa alikula mbata moja, kisha akazimika.
USHAURI SERIOUS
Matatizo anayokumbana nayo Hasheem yanatokana na Wabongo kutotambua thamani yake. Bado tunasumbuliwa na ile tabia ya wivu usiokuwa na maana.
Hata kama wewe ulikuwa maarufu kabla ya Hasheem, muhimu ni kutambua kwamba jamaa yupo daraja lingine kwa sasa.
Tulichojifunza ni kwamba watu wengine hawataki kumheshimu Hasheem kwa sababu tu walimuona jinsi alivyokuwa, anasukumwa na makonda kwenye daladala.
Jamaa ni ‘hero’ wa taifa, Watanzania wakimchukulia ni mfano wa kuigwa, anaweza kuwa njia ya vijana wengi kuelekea kwenye mafanikio. Inawezekana, wengi wanaponzwa na jinsi ‘mchizi’ anavyojichanganya na wana wa kitaa halafu anafanana nao.
**************************************************
Traki ya Njia Panda ambayo ni mali ya Barnabas ndiyo iliyomtambulisha, baada ya hapo akagonga kimya lakini sasa ameona its about time! Doreen Aurelian Ponera ‘Pipi’ anakunjuka kitaani akiwa kamili.
Pipi, ametambulisha wimbo wake wa kwanza unaokwenda kwa jina la Fisrt Time na ndani yake, hajampa mtu yeyote shavu. Amejaza vocal mwanzo mwisho!
First Time, iligongwa kwa mara ya kwanza na Radio ya Watu, Clouds FM, Alhamisi ya wiki iliyopita kisha vituo vingine vikaunga.
Pipi ni tunda lingine kutoka Tanzania House of Talent (THT).
Karibu kila binadamu ana mapenzi mema kwa wazazi wake kiasi kwamba hawezi kukaa siku kadhaa bila kuwaona au kuwajulia hali kama wako mbali zaidi, kitu ambacho ni tofauti kwa msanii Kharid Salum Kassim a.k.a Diblo, mkali wa kuchara gita na kuimba.
Alipopiga stori na safu hii hivi karibuni, Diblo ambaye hivi sasa yupo kwenye mishemishe za kuingia studio na kupiga kazi alisema kwamba, miaka 17 sasa hajawatia machoni wazazi wake ambao wanaishi Songea vijijini kwakuwa tangu amedondoka Dar es Salaam hajawahi kupata mkwanja utakaomuwezesha kufunga safari kwenda kwao ikiwemo hela ya kuwaachia.
“Huwezi kuamini huwa najisikia vibaya sana ninapowakumbuka wazazi wangu, lakini ndiyo hivyo, naomba Mungu anijalie nifanikiwe kurekodi labda muziki wangu unaweza kunisaidia kwa hilo. Naomba yeyote mwenye nia ya kunisaidia asisite kufanya hivyo,” alisema Diblo ambaye sanaa yake ya muziki amekuwa akiifanyia barabarani kwa miaka mingi bila msaada wowote.
No comments:
Post a Comment