Monday, October 25, 2010

WIKIENDA SHOWBIZ!

Mandojo
Madai Mandojo Afungwa jela Singida!
Ni masikitiko kwa wana-sanaa hasa wa Bongo Flava. Ipo stori inayovuma kwamba mchizi aliyepandisha wazimu kwa ngoma ‘Nikupe Nini’ a.k.a ‘Kanikamulie maji ya ndimu nina kiu koma’, Joseph Michael ‘Mandojo’ yupo nyuma ya nondo Singida.

Impecable sources wame-shair nasi habari kwamba msanii huyo amefungwa miaka miwili jela lakini haijabainika ni kisa gani ambacho kimempeleka ubayani.

Mshirika wa Mandojo, Precioust Juma ‘Domokaya’ last saturday aliimegea safu hii kwamba hata yeye ishu hiyo bado hajaipata fresh, anachojua ni kwamba mchizi yuko nyumbani kwao Manyoni, Singida kwa ajili ya matatizo ya kifamilia likiwemo lile la kufiwa na baba yake mzazi.

“Mi pia sijui chochote kuhusu hilo kwa sababu sijapata simu au taarifa yoyote kutoka huko, siwezi kulizungumzia hilo sana,” alisema Domo. Whole week, yaani tangu tulipodondoka kitaani Jumatatu iliyopita, tumekuwa tukipokea simu na SMS za kumwaga kuhusu habari ya kichaa kwamba hana uhuru wa kawaida kama raia wa Tanzania.

“Mandojo kafungwa miaka miwili jela, hukumu imetolewa muda mfupi uliopita,” one of impecable sources alituma SMS kwa gazeti hili. Wasanii mbalimbali wakubwa pia walimwaga data kwamba Mandojo ameingia kifungoni kwa kosa la kupigana na washkaji wengine.

Mandojo akiwa na Domokaya, walitikisa soko la Bongo Flava kati ya mwaka 2003 na 2004, walipotoka na ngoma Nikupe Nini, wakafyatua Dingi, Wanoknok ft Judith Wambura ‘Lady Jaydee’, Taswira ft Haroun Kahena ‘Inspector Haroun’, na nyinginezo kali. Kwa vyovyote vile, hii si habari njema kwa wapenzi wa muziki na sanaa yetu kwa jumla, ni vema kumuombea Mungu jamaa avuke salama katika kipindi hiki kigumu.
***********************

Eminem vs Lil Wayne Ni kitendawili cha nani Master wa Hip Hop Eminem; Mchawi wa Kufloo Lil Wayne; Sterling wa Swaga
Kuna ubishi wa muda mrefu kuhusu mkali wa ukweli wa Hip Hop aliye hai. Hatajwi marehemu Tupac Amaru Shakur (Makaveli The Don) ambaye baadhi ya mastaa wa muziki huo humwita Mfalme wa Hip Hop au Master wa Rap.

Hazungumzwi mchawi wa freestyle, marehemu Christopher Wallace ‘Notorious BIG’. Curtis Jackson ’50 Cent’ aliwahi kutajwa lakini akaondolewa, tajiri Shaun Cutter ‘Jay Z’ ni ngumu kumuondoa kwenye orodha kwa sababu ya rekodi kubwa ya mauzo aliyonayo.

Hata hivyo, ubishi mkubwa unabaki kwa ‘majanki’ wawili, kuna aliyezaliwa Oktoba 17, 1972, mwenzake Septemba 27, 1982. Mmoja ana umri wa miaka 38, mwingine alianza kuliona jua miaka 28 iliyopita, kwahiyo wana tofauti ya karibu miaka 10.

Mkubwa ni Marshall Bruce Mathers III ‘Eminem’ au Slim Shady, mdogo anaitwa Dwayne Michael Carter, Jr ‘Lil Wayne’ lakini inakubalika pia ukimwita Weezy. Hawa wapo sokoni na wanakimbiza vibaya kiasi cha kuchanganya mashabiki.

Mashabiki wa Eminem wanaamini staa wao ndiye namba moja duniani kwa sasa, wakati wale wa Weezy nao hawaachi kuvuta kamba kwao kwamba dogo anastahili taji la Ufalme wa Hip Hop. Ni stori ya mwamba ngoma!

LIL WAYNE ADAI EMINEM ANAMUOGOPA
Dogo huyo wa Cash Money, baada ya kupiga hatua kubwa kimuziki akiwa na umri mdogo, baadaye aliamua kwenda mbele zaidi kwa kutaka mpambano wa uso kwa uso na Eminem.

Kama hiyo haitoshi, Weezy akadai kuwa Eminem anaogopa kufanya naye kazi kwa sababu ya kuhofia atamfunika. “Eminem anajua nini ambacho nafanya. Nipo kwenye kiwango kizuri sana na nina mtaji wa freestyle, mashairi na swaga. Hataki kusimama na mimi, ananiogopa,” alisema Weezy katika moja ya intavyuu zake.

EMINEM AONESHA JEURI
Alipoona dogo anachonga sana, alichokifanya ni kuingia studio na kumualika Lil Wayne aingize sauti. Bonge la kolabo likachukua nafasi, jina la wimbo ni No Love.

Idea ya wimbo imetoka kwenye ngoma inayoitwa What Is Love ambayo ilikuwemo kwenye albamu ya Eminem iliyouza double-platinum ambayo inapatikana kitaani kwa jina la Recovery. No Love iliipuliwa tangu Septemba 30, 2010, ndani yake Weezy amevunja na kudondoka swaga za ukweli lakini Eminem amethibitisha kwamba linapokuja suala la kufloo, huwa habahatishi na hakamatiki.

WADAU WANAWAZUNGUMZIAJE?
Kuna maoni mbalimbali yamekuwa yakitolewa na wadau ambao ndiyo mashabiki wa wanamuziki hao. Yanamiminwa kupitia Facebook, Twiter na hata kwa kutazama video zao mtandaoni. Wingi wa maoni yao, yanatoa picha kwa kiasi gani mastaa hao walivyo na mashabiki wengi duniani lakini inapotazamwa tathmini ya jumla, Eminem anabaki kuwa juu ya Weezy kwa wapenzi na hoja.

Hata hivyo, respect ya Weezy kwa mujibu wa wadau ni jinsi alivyo mkali wa staili na swaga, wakati Eminem anabaki katika levo yake ya utaalamu wa kurap hasa katika mitindo ya ku-basti kwa haraka.

KWANINI EMINEM NI BORA?
Inapoangaliwa idadi ya nakala alizouza, moja kwa moja kurejesha macho kwa Weezy na kuwafananisha, inakuwa sawa na kulinganisha Range Rover Vogue sport na Spacio. Eminem ndiye staa wa Hip Hop anayeongoza kwa kuuza, ikiwa na maana kwamba nini Weezy, hata akina Jigga na wengineo ni tupa kule.

Ana rekodi ya kuuza zaidi ya nakala milioni 80 duniani kote na hivyo kuwekwa katika Kitabu cha Dunia cha Kumbukumbu za Guinness kama mwana-Hip Hop namba moja kwa mauzo duniani. Eminem amevunja rekodi ya Tupac ambayo aliiweka kwa kuuza kopi zaidi ya milioni 75 duniani, milioni 44 zikiwa zimenunuliwa Marekani peke yake.

EMINEM NI BABA WA 50 CENT
Baadhi ya wachambuzi hawataki kabisa kusikia Eminem akifananishwa na Weezy kwa sababu hoja moja tu kwamba staa huyo ndiye chanzo cha 50 kujulikana, inatosha kumuweka daraja lingine. Eminem ndiye aliyemtoa 50 kupitia lebo yake ya Shady Records na kufanya kazi kwa pamoja na studio ya Aftermath ya Andre Romelle Young ‘Dr. Dre.’ Pamoja na kumtoa 50, mashabiki wa Eminem, hujisikia nafuu pale staa huyo anaposhindanishwa angalau na Jigga kwa kigezo kwamba angalau viwango vinakwenda sawa.

EBWANA DAH!
Hapa tunaangalia mkali wa mademu kati yao ni nani? EMINEM Ebwana Dah, inafunua matirio kuwa Eminem amewahi kutoka kimapenzi na warembo watano wanaojulikana. Mke wake wa zamani, Kim Mathers anawekwa wa kwanza katika uhusiano wao ambao ulidumu kuanzia mwaka 1999 – 06, anayetajwa wa pili ni Brittany Murphy mwaka 2002.

Mrembo Gina Lynn alitoka naye mwaka 2003, Marni Bright mwaka 2007 na Tracy Mcnew mwaka 2008. Hata hivyo, Eminem pia amewahi kuripotiwa kutoka kimahaba na Mariah Carrey lakini baada ya kumalizana naye kitandani akamponda kwamba hana mvuto. Mkali huyo, pia alijitangaza kukwea in bed na mke wa Jigga, Beyonce Knowles.

LIL WAYNE
Ebwana Dah, lina kabrasha lenye maelezo kwamba staa huyo aliyaanza mapenzi akiwa na umri wa miaka 14, kwani kati ya mwaka 1996 hadi 2006, alitoka kimapenzi na Antonia Carter.

Mwaka 2003-05, alikwenda sawa na Christina Milian, akatulia na Nivea B. Hamilton-Nash kati ya mwaka 2003 hadi 2009, akamegana kisela na Katrina Laverne Taylor ‘Trina’ mwaka 2005 hadi 2006. Alitoka na Sarah Bellew kati ya mwaka 2005 hadi 2008 halafu mwingine anayeunga listi yake ni Lauren London.

compiled by mc george/wikienda

No comments: