Thursday, December 9, 2010

MPIGIE KURA DIAMOND NAYE AKAMATE TUZO ZA MTV!

Msanii Diamond akila pozi na kupewa changamoto na Queen wa Pop, Britney Spears mjini London hivi karibuni . Britney aliwahi kuwa mshindi wa MTV Awards miaka iliyopita. Diamond alikuwa katika ziara ya muziki nchini Uingereza hivi karibuni iliyojulikana kama Urban Tour na kupata nafasi adimu ya kupiga picha na msanii mwenzake wa kimataifa.

URBAN PULSE CREATIVE Inawaomba na kuwasihi watanzania wote popote walipo kumpigia kura Mtanzania mwenzetu, Ndugu Yetu, rafiki Yetu, Msanii wetu mpendwa Diamond, ambaye amebahatika kuwa miongoni mwa wasanii wachache waliochaguliwa kuwania Tuzo za MTV (MAMA 2010) Zitakazo fanyika Nigeria Jijini Lagos Jumamosi hii, Dec 11, 2010. Hivyo basi, watanzania na wadau wote wa muziki mnaombwa sana kupiga kura ili Kumwenzesha Diamond ashinde tuzo hii muhimu iweze kuja Tanzania ili kuiwezesha nchi yetu kujulikana zaidi ulimwenguni na pia kuleta HESHIMA kubwa kwa kila MTANZANIA.

Namna ya kupiga Kura ni kama ifuatavyo:1. Kwa njia ya simu unaweza kupiga kura yako kwa kuandika neno BNA DIAMOND kisha tuma text kwenda namba 6262, kwa walio nje yaTanzani tuma text 15726.

2. Kutumia Mtandao, fungua tovuti hii http://www.mtvbase.com/splash/mama/ bonyeza mtv mama halafu ingia ndani ya nominees. Tunaomba umpigie kura as the best New Act. Tafadhali fanya sehemu yako na mwambie mwenzako. Asanteni sana na Mungu awabariki.

Diamond Platinumz
akishirikiana na
URBAN PULSE CREATIVE

2 comments:

Simon Kitururu said...

Kura yangu Kapata!

Anonymous said...

KURA TUTAMPA ILA ACHENI KAMBA HUYO SI BRITNEY HALISI BALI NI WAXWORK ILIYOPO KATIKA HALL LA MADAMME TUSSAUDS LONDON.

Angalia this site: http://news.xinhuanet.com/english/2009-02/17/content_10831608.htm