Saturday, October 6, 2012

AFRICA MAGIC KWA KUSHIRIKIANA NA MULTICHOICE YAANDAA TUZO KWA WAIGIZAJI NA WATENGENEZAJI BORA WA FILAMU BARANI AFRIKA.

Pichani Juu na Chini ni Meneja wa MNET Ukanda wa Afrika Mashariki Bi. Risper Muthamia wakati wa kutangaza rasmi kutolewa kwa Africa Magic Viewers Choices Awards (AMVCA), ambapo amesema zitawashirikisha Wasanii, Waandaji na Waandishi wa Filamu kutoka Barani Afrika zitakazofanyika Lagos nchini Nigeria tarehe 9 Machi 2013.
Bi. Risper Muthamia amesema kuwa Filamu zote zilizotengenezwa kwa ajili ya Televisheni na mfululizo wa vipindi vya Luninga (Series) zinaweza kuwasilishwa kuwania tuzo hizo iwapo zilitengenezwa na kurushwa hewani au kuonyeshwa hadharani katika kipindi cha kati ya May 1, 2011 hadi April 30, 2012.
Aidha amefafanua kuwa Filamu au vipindi vitakavyoshiriki katika tuzo hizo viwe ni katika lugha ama ya Kiingereza, Hausa (Nigeria), Swahili au Yoruba na kusisitiza kuwa hakuna Lugha nyingine itakayokubalika.
Ameongeza kuwa Filamu na Sinema zilizotengenezwa kwa ajili ya Televisheni zinapaswa kuwa na urefu wa kati ya Dakika 60 mpaka 90 wakati Mfululizo wa vipindi vya Luninga (Series) ni kwa muda wa dakika 30 mpaka 60. Wasanii wamekumbushwa kuwa ili kuweza kushiriki katika tuzo hizo wanapaswa kuwasilisha nakala 6 za DVD za filamu zao.
Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania Barbara Kambogi akizungumza katika semina fupi ya wadau wa tasnia ya Filamu nchini pamoja na waandishi wa habari na kusisitiza kuwa wasanii watakaopelekea kazi zao wahakikishe kuwa sio za kuiga na zina hati halali ya kusajiliwa na COSOTA.
Msanii wa filamu nchini almaarufu kama Mtitu akitoa maoni yake kuhusiana na tuzo AMVCA zilizoanishwa na Africa Magic kwa kushirikiana na Multichoice kwa ajili ya kutambua mchango wa wasanii wa bara la Afrika kwa lengo la kukuza sekta ya filamu Kimataifa.
Wasanii wa filamu wakisimama kwa dakika moja kumkumbuka Aliyekuwa msanii maarufu wa filamu Tanzania na Afrika kwa Ujumla aliyefariki dunia ghafla Marehemu Steven Kanumba.
Msanii wa filamu Cloud naye akichangia mawazo yake wakati wa semina hiyo.
Rais wa Shirikisho la Filamu Nchini (TAFF) Bw. Simon Mwakifamba akiwasisitiza wasanii na watengenezaji wa filamu kuhakikisha zinakuwa na maudhui ya Kiafrika na ubora unaokubalika.
Bw. Mwakifamba amewataka Watanzania kujenga utamaduni wa kupenda filamu za nyumbani na kushiriki katika kuzipigia kura pindi zinapokuwa katika mashindano ya aina mbalimbali kama itakavyokuwa katika Africa Magic Viewers Choice Awards (AMVCA).
Meneja wa MNET Ukanda wa Afrika Mashariki Bi. Risper Muthamia akielezea kuwa taarifa zaidi kuhusiana na tuzo hizo zinapatikana katika tovuti ya Africa Magic ambayo ni www.africamagic.tv na kuwa kiingilio cha kushiriki katika tuzo hizo ni bure na mwisho wa kuwasilisha fomu za ushiriki ni Oktoba 31, 2012. Kulia ni Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania Furaha Samalu.
Baadhi ya wasanii wa filamu nchini waliohudhu8ria semina fupi iliyohusiana na Africa Magic Viewers Choice Awards (AMVCA). Kutoka kushoto ni Msanii Sajuki akiwa amembatana na mkewe na msanii nguli Dkt. Cheni.
Mchekeshaji na Msanii wa Filamu Steven Nyerere akitoa maoni yake kuhusiana na tuzo hizo.
Meneja Masoko wa Mutichoice Tannzania Bi. Furaha Samalu sambamba na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo Barbara Kambogi (wa kwanza kulia).
Yusuf Mlela na msanii mwenzake.
Msanii nguli katika sanaa ya maigizo na filamu hapa nchini almaarufu kama Bi. Mwenda.
Charles Baba naye alikuwepo.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Steps Entertainment Bw. Jai (wa pili kushoto) ambao ni wasambazaji wa filamu nchini akizungumza na maafisa wa kampuni ya Multichoice.
Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania Bi. Furaha Samalu akibadilishana mawazo na msanii wa Filamu nchini maarufu kama Cloud.
Meneja Uhusiano wa Multichoice Tanzania Barbara Kambogi akiteta jambo na mmoja wa washiriki wa semina hiyo iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam kwa lengo la kufafanua vigezo vitakavyotumika wakati Africa Magic Viewers Awards (AMVCA) zinazotarajiwa kufanyika March 9, 2013 Lagos Nigeria.

No comments: