Sehemu ya umati watu waliojitokeza kila kona jiji la Dar na kwingineko kuwashuhudia wasanii mbalimbali wakitumbuiza kwenye jukwaa la tamasha la Serengeti Fiesta 2012,akiwemo Mwanamuziki wa kimataifa kutoka nchini Marekani,Rick Ross.
Wasanii wa kundi la Wanaume TMK,likiongozwa na Mh Themba sambamba na Chege Chigunda wakilishambulia jukwaa vilivyo usiku huu kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2012,linaloendelea hivi sasa katika viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar.uwanja wa Lidaz Club hapatoshi kabisa usiku huu.
Nyomi la Watu ile balaa usiku huu.
Wasanii wa kikundi cha Makomando kutoka THT wakionesha umahiri wao wa kucheza jukwaa.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Dyana pichani akionesha mbwembewe zake kabla ya kukamata kipaza sauti,mbele ya umati mkubwa uliojitokeza kwa wingi usiku huu ndani ya viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar
Msaniii mahiri wa kizazi kipya,Barnaba Boya kiimba jukwaani huku Dyana na skwadi lake wakionesha mbwembwe zao kama kawa.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Barnaba Boy akiimba jukwaani usiku huu
Mmoja wa wshindi wa shindano la Serengeti Supa Nyota 2012,Youk Killer akishusha mistari yake nguvi usiku huu,huku shangwe na vigele vigele vikiwa vimetawala.
Mashabiki wakishangweka usiku huu vilivyo.
Mmoja wa washindi wa shindano la Serengeti Supa Nyota 2012,Jo Maker akifloo jukwaani. .
Baadhi ya mashabiki wakijiachia vilivyo usiku huu ndani ya tamasha la Serengeti Fiesta 2012
Mmoja wa wshindi wa shindano la Serengeti Supa Nyota 2012,NeyLee akiimba jukwaani .
Baadhi ya wasanii kutoka nyumba ya vipaji THT wakiamsha amsha usiku huu wakati tamasha la Serengeti Fiesta 2012 likiendelea huku mashabiki na wapenzi wa tamasha hilo wakiendelea kumiminika usiku huu ndani ya viwanja vya Lidaz Club,jijini Dar.
Mmoja wa wasanii chipukizi kutoka kwa THT,akiimba kwa hisia mbele ya umati mkubwa wa watu (haupo pichani),uliojitokeza kushuhudia wasanii wa hapa nyumbani na nje wakitumbuiza katika jukwaa moja usiku huu.
Mmoja wa wasanii chipukizi akinogesha jukwaa la Serengeti Fiesta 2012 usiku huu
The Wacko Jako wa bongo akifanya vitu vyake jukwaani usiku huu
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar na vitongoji vyake wakiwa tayari ndani ya viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar usiku huu wakati wa tamasha la Serengeti Fiesta likiendelea kurindima,huku wakimsubiri kwa hamu mwanamuziki wa Kimataifa kutoka nchini Marekani,Rick Ross ambaye anatarajia kukamua usikuu huu.
No comments:
Post a Comment