Monday, June 15, 2015

NASSAR AISHUKURU BENKI YA NMB KWA MISAADA INAYOENDELEA KUTOA

Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassar akifurahia msaada wa madawati toka Benki ya NMB ,wengine ni viongozi kutoka katika benki hiyo pamoja na viongozi waliokuwa wakiiwakilisha serikali. 
Meneja wa Benki ya NMB tawi la Usa River,Bernadeta Mmary akikabidhi msaada wa madawati kwa mwakilishi wa afisa elimu ,Jumanne Masuke uliotolewa na benki kwa shule ya msingi ,Sura iliyopo kijiji cha Songoro wilayani Arumeru.
Mbunge Joshua Nassar akizungumza wakati wa hafla fuoi ya kukabidhi msaada wa madawati uliotolewa na Benki ya NMB kwa ajili ya shule ya msingi Sura iliyopo kijiji cha Songoro wilaya ya Arumeru.
Baadhi ya wanafunzi wakiwa wameketi katika madawati yaliyotolewa na Benki ya NMB.
Baadhi ya wazazi wenye watoto katika shule ya msingi Sura iliyopatiwa msaada wamadawati na Benki ya NMB.
Meneja wa NMB tawi la Usa River ,Bernadeta Mmary akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo wa madawati.
Makilishi wa Afisa elimu wa wilaya ya Meru,Jumanne Masuke akizungumza katika hafla hiyo.
Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Sura ,Raphael Akyoo akizungumza katika hafla ya kukabidhiwa madawati.
Mwakilishi wa Benki ya NMB kanda ya Kaskazini ,Helen Binarita akizungumza wakati wa hafla hiyo iliyofanyika shuleni hapo.
Mbunge Nassar pamoja na viongozi wa benki ya NMB wakiwa katika picha ya pamojamara baada ya kukabidhi msaada wa madawati.
Moja ya darasa katika shule ya msingi Sura likiwa halina madawati.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.

No comments: