Monday, June 15, 2015

UN YAISIFU TANZANIA KUWA MSTARI WA MBELE KUTETEA ALBINO

UN 12
Baadhi ya watu wenye ulemavu wakipita na mabango yenye ujumbe katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Arusha kwa maandamano kwenye maadhimisho ya Siku yao ambayo inalenga kutoa elimu ya kupinga matendo maovu wanayofanyiwa na watu wenye nia mbaya.(Picha na modewjiblog)
Na Mwandishi wetu, Arusha
MRATIBU Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mkurugenzi wa Shirika la Mpango wa maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodgriguez amepongeza Tanzania kwa kuwa mstari wa mbele kushawishi dunia siku ya kukumbuka watu wenye ulemavu wa ngozi duniani.
Alisema dhana ya Juni 13 ilianzia Tanzania kwa mshikamano kati ya serikali ya Tanzania na mashirika yasiyo ya kiserikali kama Shirika la Under the same sun (TAS).
Alisema kutokana na bidii walizoonesha Novemba 18,2014, Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa lilipitisha siku hiyo kuadhimishwa duniani kote kila ifikapo Juni 13
Akihutubia kabla ya rais Jakaya Kikwete ambaye alikuwa mgeni rasmi kuzungumza, Rodgriguez alisema dunia inapaswa kuangalia kwa makini maisha ya walemavu wa ngozi na kuzuia ukatili dhidi yao.
Alisema pamoja na haja ya kuongeza ufahamu wa watu juu ya masuala ya ualibino na maalbino ni vyema jumuiya ya kimataifa kuhakikisha kwamba kila mwanamke, mwanamume na mtoto wanatendewa kwa usawa na kwa heshima.
Alisema kutokana na haja hiyo Umoja wa Mataifa umekuwa ukifanyakazi na serikali ya Tanzania kuboresha maisha ya watu wake kwa kusaidia kuimarisha mfumo wa mahakama, masuala ya wakimbizi na masuala ya utoaji haki.
Alisisitiza kuwa kuwapo kwa haki, usawa na utu kutahakikisha kuwapo kwa amani na usalama kwa jamii zenye ulemavu wa ngozi.
Alisema kwa sasa kuna woga mkubwa kwa jamii ya ulemavu wa ngozi kutokana na chuki, unyanyapaa, mashambulizi ya kutisha, mauaji na kugeuzwa kuwa bidhaa huku wakiuuawa kwa sababu za matambiko ya kutafuta utajiri.
Mratibu huyo alisema kwamba taifa na jamii ya binadamu wote wanatakiwa kushirikiana katika kuzuia ukatili kwa wenye ulemavu na pia kuwasaidia kukabilina na mazingira yao magumu hasa upatikanaji wa vifaa vya kuwakinga na madhara ya jua.
Alitaka pia jamii kuelimishwa kuhusu mtiririko wa vinasaba vinavyosababisha ulemavu wa ngozi na kupambana na ubaguzi na tishio la maisha kwa kutoa mafunzo mbalimbali.
Aidha alisema Umoja wa Mataifa utaendelea kufanya kazi na wanachama wa taasisi mbalimbali zisizo za kiserikali na Serikali kuimarisha haki za binadamu .
UN 10
Baadhi ya watu wenye ulemavu wakipita na mabango yenye ujumbe katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Arusha kwa maandamano kwenye maadhimisho ya Siku yao ambayo inalenga kutoa elimu ya kupinga matendo maovu wanayofanyiwa na watu wenye nia mbaya.
UN 11
Baadhi ya watu wenye ulemavu wakipita na mabango yenye ujumbe katika mitaa mbalimbali ya Jiji la Arusha kwa maandamano kwenye maadhimisho ya Siku yao ambayo inalenga kutoa elimu ya kupinga matendo maovu wanayofanyiwa na watu wenye nia mbaya.
UN 6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Jakaya Kikwete akihutubia wananchi waliohudhiria maadhimisho hayo kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
UN 1
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa(UN) na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) hapa nchini, Alvaro Rodriguez akihutubia katika Maadhimisho ya Siku ya wenye Ualbino yaliyofanyika leo kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
UN 3
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa(UN) na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) hapa nchini, Alvaro Rodriguez akipongezwa na Rais Jakaya Kikwete baada ya kutoa hotuba yake katika Maadhimisho ya Siku ya wenye Ualbino yaliyofanyika leo kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
UN 4
Balozi wa Canada hapa nchini, Alexandre Leveque akihutubia katika Maadhimisho ya Siku ya wenye Ualbino yaliyofanyika leo kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
UN 5
Mwenyekiti wa wenye ulemavu wa ngozi nchini(TAS), Ernest Kimaya akitoa nasaha zake.
UN 7
Naibu Waziri wa Afya, Dk.Kebwe Steven Kebwe akitoa nasaha zake.
UN 8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk Jakaya Kikwete akiwapongeza watoto wenye Ualbino wanaofadhiliwa na USAID chini ya mpango wa Tuwalee.
UN 13
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk Jakaya Kikwete akiagana na Balozi wa Canada hapa nchini, Alexandre Leveque baada ya maadhimisho hayo, kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa(UN) na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) hapa nchini, Alvaro Rodriguez na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda.

No comments: