Samsung GALAXY S 7
Samsung
Na Mwandishi Wetu , Dar Es Salaam,
Kampuni ya simu ya
Samsung imevuka mipaka kwa mara nyingine tena kwa ujio wa simu za galaxy
smartphone. Msimu huu, sio tu kwamba Samsung inazindua simu mpya bali inazindua
mfumo mpya wa kufikiri nini hasa simu inaweza kufanya kwa jinsi
tunavyoichukulia teknolojia yetu. Kwa Tanzania, Samsung inawapa watumiaji wake
sababu za msingi za kuweka oda ya simu mpya ya Galaxy S7.
Simu za Galaxy S7 na
S7 Edge zitakufanya ufikiri tena uwezo na vitu gani simu inaweza kufanya.
Kufuatia S6 kushinda karibu tuzo zote za simu bora za smartphone kwa mwaka
2015, mwezi March kampuni ya Samsung imedhamiria kuzindua simu iliyokuwa
ikisubiriwa sana katika matoleo ya galaxy. S7, simu iliyosheneni program mpya
zaidi kuliko toleo lolote la Galaxy inayokuja na kasha imara, kioo chenye inchi
5.5 chenye skrini yenye mwonekano bora. Samsung Galaxy S7 ni simu ya kwanza
yenye teknolojia ya kiwango cha juu cha picha (dual-pixel) na pia yenye uwezo
wa kupiga picha ya mbali. Inakupa fursa ya kupiga picha kwa zote kwa kiwango cha ubora wa juu katika
sehemu zenye mwanga mdogo/giza. Simu zetu huwa tunaenda nazo kila mahali
isipokuwa sehemu zenye maji. Samsung S7 imefungua ulimwengu wa kutumia simu yako
ukiwa unanyeshewa na mvua au kwenye bwawa la maji. Kwa betri inayodumu muda
mrefu, Samsung S7 inakupa uwezo wa kuitumia muda wa siku nzima na zaidi ya
hapo.
“Tunaamini katika
ulimwengu wenye mafanikio, spidi, na furaha zaidi. Tunajitahidi kufikia lengo
hilo kwa ujio wa Galaxy S7 na Galaxy S7 edge kwa kuzingatia dizani murua yenye
utendaji wa hali ya juu wa kukupa ujuzi
bora wa matumizi ya simu” alisema DJ
Koh, Raisi wa mawasiliano na biashara wa kampuni ya simu za Samsung. “Tunawawezesha
watumiaji kwa teknolojia ili kuwasaidia kujifunza mengi katika maisha na
tutaendelea kusukuma gurudumu hili kwa lolote litakalowezekana.”
”Maisha ya watumiaji
simu nchini Tanzania yanabadilika kwa haraka, mahitaji na matarajio yao ya
kutumia simu zenye ubora wa hali ya juu yanaongezeka. Mfumo wa kuopereti ndio
sababu pekee pale unapojadili simu mpya na za kisasa kwa sababu unamadhara
makubwa katika ufanyaji kazi wa simu katika matumizi, na urahisi wake wa
uendeaji. Wigo wa program katika simu ya Samsung Galay S7 unakupa uwezo wa usio
na kifani wa matumizi ya simu kwa watumiaji wote”. Aliyasema hayo Rayton Kwembe meneja bidhaa kutoka kampuni
ya Samsung Tanzania.
Simu za “smartphone”
ni kwa ajili kufurahia habari na taarifa wakati bado unawasiliana. Mtu anaweza
kuangalia filamu, kucheza michezo ya kwenye simu, na kuangalia picha kwa
kupitia skrini ya simu yako hivyo unahitaji simu yenye mwonekano mzuri na
mkubwa. Kioo cha simu kikubwa na angavu cha Galaxy S7 kina lengo la kuwapa
burudani watanzania.
Nafasi ndogo ya
kuhifadhi kumbukumbu na usalama umekuwa ni ishu kubwa kwa watanzania na
watumiaji wa simu, kwa ujio wa S7 kutakuwa hamna tena matatizo kama hayo na
uwepo wa kuweka kidole kama nywila itatatua changamoto ya usalama. Betri
inayokaa muda mrefu na spidi ya ufanyaji kazi ni zawadi kutoka S7.
Simu nyingi nyingi za
kawaida huwa zinakuwa na uwezo wa kawaida katika matumizi ya intaneti, intaneti
inakuwa ngumu kuitumia kwa sababu ya skrini ndogo ya simu na kava pia. Kwa simu
yenye nguvu katika utendaji na program inayoendana na simu, S7 itatumika
kuwezesha kazi zote za kimtandao.
Kuanzia tarehe 4 mwezi
March, kampuni ya simu ya Samsung itakuwa inafanya maonyesho ya Galaxy S7
katika maduka ya Samsung Mlimani City, City Mall, na Jm Mall pamoja na maduka
ya Vodacom ya Mliman City na Samora avenue. Kuweka oda kunaweza pia kufanyika
kwa kupiga simu namba 0766960517 au kupitia tovuti http://www.samsung.com/africa_ en/home/.
Maonyesho hayo ya Samsung yatahusisha kifaa chao kipya cha Gear VR- kinachokupa
uwezo wa kuona vitu halisi, kitakachotumika kama bendera katika toleo hili kama
ilivyokuwa kwa Gakaxy S6, S6 edge, S6 edge+ na Note 5 kwa ajili ya kuonyesha
picha halisi. Gear VR inampa mtumiaji aliyevaa kifaa hicho usoni ujuzi wa
tofauti ukilinganisha na anayeangalia moja kwa moja kwenye Tv kwa sababu
maudhui yote ya unachoangalia yanachukuliwa na simu yako.
Maduka hayo yatakuwa yanachukua oda za samsung galaxy S7 wale wote
watakao weka oda watapatiwa spika ndogo za masikioni za Samsung zinazotumia
Bluetooth ambazo huwa zinajulikana kwa wengi kwa jina la Samsung level U. spika
hizi zina vifaa vya kisasa vya kuwekwa shingoni ili kushikilia vizuri spika
hizo ndogo masikioni. Zenye ukubwa wa 12mm spika hizo zitakupa sauti yenye
kiwango cha hali ya juu. Kipaza sauti kisicho na mwangwi na chenye ubora wakati
wa kuongea na simu. Kwa ajili ya kuweka oda ya simu iliyosubiriwa muda mrefu ya
Samsung galaxy S7, bei ya rejareja ni Tzs 1.68m (pamoja na vat)
na S7 edge kwa Tzs 1.89m (pamoja na vat).
Kampuni ya Samsung imeingia ubia na Vodacom katika kifurushi cha
intaneti kwa ajili ya ujio na promosheni za Samsung Galaxy S7 ambapo watanzania
watafurahia 10 GB za intaneti bure kwa kila Samsung S7.
Kuhusu Kampuni ya vifaa vya
Samsung.
Kampuni ya vifaa vya Samsung ni kiongozi ulimwenguni katika teknolojia,
kufungua fursa mpya kwa watu wote kila mahali. Kwa kupitia teknolojia ya hali
ya juu na ugunduzi mbalimbali, kampuni ya Samsung inahamasisha ulimwengu na
kuleta matumaini ya mabadiliko katika mitazamo na teknolojia zinazolenga katika
televisheni, simu, vifaa vya kuvaa, kamera vifaa vya umeme, mtandao, vifaa vya
afya na LED. Samsung imeajiri zaidi ya wafanyakazi 319,000 katika nchi 84 na
inafanya mauzo ya mwaka dola bilioni 216.7 kujifunza zaidi tembelea www.samsung.com.
No comments:
Post a Comment