Saturday, June 25, 2016

BARAZA KUU LA KWANZA LA WAFANYAKAZI WA TAZARA LAZINDULIWA RASMI LEO DAR

DSC_8172Dada Regina Tarimo Afisa uhusiani wa TAZARA-Tanzania, akiwakaribisha wajumbe wa Baraza hilo jipya kwenye mkutano maalum wa uzinduzi wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa TAZARA unaondelea jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Lamada, leo Juni 25.2016.
DSC_8175
Baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa TAZARA wakifuatilia mkutano huo unaondelea jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Lamada, leo Juni 25.2016.

DSC_8178
Baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa TAZARA wakifuatilia mkutano huo unaondelea jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Lamada, leo Juni 25.2016
DSC_8196
Baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa TAZARA wakifuatilia mkutano huo unaondelea jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Lamada, leo Juni 25.2016
DSC_8185 DSC_8187Baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa TAZARA wakifuatilia mkutano huo unaondelea jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Lamada, leo Juni 25.2016
DSC_8201Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama Huru vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Nicholas Mgaya akisoma taarifa namna ya TUCTA inavyofanya kazi na Mabaraza ya wafanyakazi sehemu za kazi.
DSC_8190Baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa TAZARA wakifuatilia mkutano huo unaondelea jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Lamada, leo Juni 25.2016
DSC_8182Baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa TAZARA wakifuatilia mkutano huo unaondelea jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Lamada, leo Juni 25.2016
DSC_8213Katibu Mkuu wa Wizara hiyo upande wa Uchukuzi, Dk Leonard Chamuriho akisoma hutuba hiyo ya ufunguzi kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo, Profesa Makame Mabarawa.
DSC_8181Baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa TAZARA wakifuatilia mkutano huo unaondelea jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Lamada, leo Juni 25.2016
DSC_8179Baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la Wafanyakazi wa TAZARA wakifuatilia mkutano huo unaondelea jijini Dar es Salaam katika hoteli ya Lamada, leo Juni 25.2016
DSC_8222
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo upande wa Uchukuzi, Dk Leonard Chamuriho (mbele) akisoma hutuba hiyo ya ufunguzi kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo, Profesa Makame Mabarawa.
DSC_8223Katibu Mkuu wa Wizara hiyo upande wa Uchukuzi, Dk Leonard Chamuriho akisoma hutuba hiyo ya ufunguzi kwa niaba ya Waziri wa Wizara hiyo, Profesa Makame Mabarawa.
DSC_8249Katibu Mkuu wa Wizara hiyo upande wa Uchukuzi, Dk Leonard Chamuriho(wa pili kutoka kulia) akipiga picha ya pamoja na viongozi wa juu wa wafanyakazi wa TAZARA. DSC_8252 DSC_8261Katibu Mkuu wa Wizara hiyo upande wa Uchukuzi, Dk Leonard Chamuriho (Katikati) akipiga picha ya pamoja na wajumbe wa Baraza jipya la Wafanyakazi wa TAZARA. (Picha zote na Andrew Chale,Modewjiblog).
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa. Makame Mbarawa (MB) amezindua rasmi Baraza Kuu la kwanza la Wafanyakazi wa Mamlaka ya reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA) tukio lililofanyika mapema leo Juni 25.2016, Jijini Dar es Salaam.
Akisoma hutuba ya ufunguzi wa Baraza hilo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo upande wa Uchukuzi, Dk Leonard Chamuriho kwa niaba ya Waziri Profesa Mbarawa, Amelitaka Baraza hilo kufanya kazi kwa moyo mmoja katika hali ya kuifufua TAZARA kiutendaji na ufanisi kama ilivyokuwa zamani.
Akisoma hutuba hiyo, aliwapongeza viongizi wa wanaounda Mamlaka hiyo akiwemo Mhandisi Bruno Ching’andu kwa kuteuliwa kwake kuongoza Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia na viongozi wengine pamoja na wafanyakazi wote.
Ambapo alisema kuwa, ni dhahiri hatua ya leo imefikiwa baada ya jitihada kubwa na hasa tukitilia maanani hali ya kifedha ambayo TAZARA inapitia katika kipindi hiki. Hivyi kuwapongeza kwa uamuzi huo kwani Mabaraza yana umuhimu mkubwa katika maeneo ya kazi na yameonyesha mafanikio makubwa kila yalipoanzishwa kwani yameweza kuongeza uhusiano mwema kati ya Manejimenti, Vyama vya Wafanyakazi na wafanyakazi kwa upande mwingine.
“Mabaraza haya ni dhana ya ushirikishwaji ikiwa na maana kuwapatia wafanyakazi fursa ya kushauri juu ya masuala ya utendaji kazi, sera za taasisi, ufanisi wa kazi, mazingira ya kazi, ustawi wa wafanyakazi katika elimu, nidhamu, vyeo, pamoja na motisha kwa wafanyakazi. Pia dhana hii ya ushirikishwaji ni kwa mujibu wa sheria ya Utumishi wa Umma Na. 8 ya mwaka 2002 na kanuni zake za mwaka 2003 kifungu cha 108.
Pia ni kwa mujibu wa Sheria ya majadiliano katika Utumishi wa Umma Na. 19 ya mwaka 2003 na kanuni zake za mwaka 2005. Pia Sheria ya ajira na mahusiano kazini ya mwaka 2004 na kanuni zake za mwaka 2007 kifungu Na. 73 (1 - 3).
Taarifa niliyopewa ni kwamba kikao hiki cha sasa cha Baraza kitapata fursa ya kuijadili taarifa ya kazi ya Mamlaka kwa mwaka 2015/2016, kuupitia mpango kazi kwa kipindi cha 2016/2017 na pia bajeti ya mapato na matumizi ya Mamlaka kwa kipindi cha mwaka 2016/2017. Kwa maana hiyo hiki ni kikao muhimu sana kwa mustakabari wa Mamlaka ya TAZARA.
Wajumbe wote ninawaomba muwe makini sana kuelewa hayo malengo na kuweza kutafsiri kwa usahihi ili muweze kuyawakilishe hali halisi kwa wafanyakazi wenzenu kwa ili malengo yapate kutimizwa. Ninyi mtakuwa kiungo muhimu sana katikakufanikisha swala zima la kuleta matumaini mapya.
Kwa kuwa Mamlaka hii ni alama ya ushirikiano baina ya Tanzania na Zambia imeendelea kuwa muhimu kwa nchi zetu. Napenda kuwakumbusha wajumbe wote kwamba wajibu wenu kwa sasa ni kuhakikisha Mamlaka inarudi katika hali yake ya zamani ilipokuwa ikijiendesha yenyewe kwa kutimiza wajibu wake wa kulipa mishahara kwa wafanyakazi,kulipa kodi Serikalini, michango ya wafanyakazi katika mufuko ya jamii ..
Na kwa njia hii pekee itayorudisha imani upya kwa wateja ambao wamejiondoa kwa kipindi sasa hali iliyopelekea hali ya Mamlaka kimapato kudhoofika.
Kwa kumalizia, napenda nitoe rai kwa uongozi wa Mamlaka na wa vyama vya Wafanyakazi kuwa mkutano huu uwe ni mwanzo muendelezo wa mikutano mingine kadri kanuni inavyoagiza ili kuongeza tija na utulivu. Mahali hapa ni fursa ya kuelezana, kukosoana na kuwekana sawa kwa manufaa ya TAZARA na Umma wote wa Tanzania na wa Zambia pamoja na nchi jirani wanaotumia reli hii kwa namna moja au nyingine.
Mwisho nawatakia mkutano wenye mafanikio na pia napenda kutangaza kwamba Baraza hili nimelizindua rasmi. Ahsanteni!

No comments: