Samwel Mwakalobo Bwanaharusi ambaye ameingia mitini muda mchache kabla kuingia kanisani kufunga ndoa katika kanisa la K.K.K.T Isanga jijini Mbeya. |
Na JamiiMojaBlog ,FahariNews
Mwisho wa mwaka 2016 huenda ukamaliza na kituko cha aina yake
katika Mitaa ya Isanga Jijini Mbeya Mkoa
wa Mbeya mara baada ya bwanaharusi
kuingia mitini masaa machache kabla ya kufunga ndoa.
Tukio hilo la aina yake limeibua maswali mengi kwa ndugu
jamaa na marafiki ambao walikuwa tayari kwa maandalizi ya kuhudhuria harusi
hiyo kuanzia kanisani hadi ukumbini.
Imeelezwa kuwa mipango yote ya harusi ilifanyika kwa pande
zote mbili kushiriki kwa kufuata
taratibu zote zinazotakiwa kufuatwa hadi hatua ya mwisho ya kuingia kanisani
ambapo kama kawaida ndugu jamaa wote walihudhuria kanisani kwa lengo la
kushuhudia tukio hilo .
Tukio rasmi lilianza majira ya saa 7 mchana katika kanisa la
K.K.K.T Usharika wa Isanga jijini Mbeya
Desemba 16 ambapo kama kawaida
Bibi harusi akiongozana na wapambe wake akifuata na msafara wa magari zaidi ya
manne akitokea Saloon na kuingia
kanisani hapo.
Baada ya bibi harusi kuingia kanisani tayari kwa kufunga ndoa
hiyo taarifa zilianza kuenea kuwa
bwanaharusi hayupo kanisani hapo na hajulikani mahali alipo.
Kadri muda ulivyozidi kwenda bila bwana harusi kufika
kanisani hapo baadhi ya Ndugu, jamaa na watu
waliohudhuria harusi hiyo walianza kuhoji ambapo kwa muda huo yalipita zaidi ya
masaa 4 bila chochote kuendelea kanisani hapo.
Kadi ya mualiko kwa ajiliya sherehe |
Bibi harusi Given
Mgaya Mkazi wa Isanga jijini Mbeya |
No comments:
Post a Comment