Monday, April 3, 2017

MAKAMU WA RAIS CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM (DARUSO) SHAMIRA MSHANGAMA AKUTANISHA WADAU KUJADILI DHANA YA “MWANAMKE NA UONGOZI” UDSM

Aliyekuwa Mgeni Rasmi katika kongamano hilo lililo andaliwa na Makamu wa Rais wa Serikali ya wanafunzi wa  Chuo Kikuu cha Dar es salaam Bi. Shamira Mshangama Mh. Sophia Mjema akitoa nasaha zake kwa wote waliohudhuria katika kongamano hilo lililofanyika katika Ukumbi wa Nkurumah Chuo kikuu cha Dar es salaam.
  Makamu wa Rais wa Serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es salaam Bi. Shamira Mshangama akieleza kwa ufupi juu ya Kongamano hilo na Kumkaribisha
Mkurugenzi wa Maswala ya Jinsia Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Dkt. Kafanabo
Mkurugenzi wa Maswala ya Jinsia Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Dkt. Kafanabo akielezea kwa undani juu ya jinsia na uongozi katika kongamano hilo
 Mkurugenzi Mkazi wa Asasi ya Kiraia ya Global Peace Foundation(GPF) nchini Tanzania Bi. Martha Nghambi akielezea shughuli za asasi hiyo na nafasi ya mwanamke katika uongozi.
Meneja wa Benki ya NMB PLC tawi la Chuo Kikuu cha Dar es salalaam Bi. Rehema Mwibura akielezea safari yake ya uongozi mpaka hapa alipofikia sasa na kuwaatha vijana wakike wasikate tamaa kwa kuwa wanaweza.
 Mwanachama wa zamani wa USRC Bi. Yunge Kanuda akiwasihi vijana wanawake kuwa wanayo nafasi ya kugombea ngazi mbalimbali za uongozi hivyo wanatakiwa wathubutu ili waweze kushika nyadhifa mbalimbali.
Washiriki wa Kongamano hilo wakifuatilia kwa makini mijadala mbalimbali inayoendelea
Aliyekuwa Spika wa Bunge la USRC kwa mwaka 2014/2015 Protus Petro akielezea juu ya uongozi 
Aliyekuwa Makamu wa Rais wa Serikali ya wanafunzi Chuo Kikuu cha Dar es salaam Irene Ishengoma na aliyeshiriki Shindano la Maisha Plus 2016 akielezea mambo mbalimbali yanayowahusu wanawake na kuwasihi kuto bweteka kwa kuwa wanaweza.
 Baadhi ya Washiriki wa Kongamano hilo wakiuliza maswali na kuchangia mawazo katika Kongamano hilo.
 Mwanzilishi na Rais wa Taasisi ya wanafunzi wanawake kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam Consolata Chikoti akifuatilia kwa makini mijadala ikiendelea.
 Mh. Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema (wa nne kutoka kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na waliokuwa wazungumzaji wakati wa Kongamano hilo.
  Mh. Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema (wa nne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi ya Kongamano la Wanawake na Uongozi
  Mh. Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema (wa nne kutoka kushoto) kwa waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya viongozi wa Serikali ya wanafunzi Chuo kikuu cha Dar es salaam.
 Picha ya pamoja ya viongozi kutoka maeneo mbalimbali ikiwa ni Asasi,vyuo na shule shule mbalimbali
Washiriki wakiwa katika Kongamano hilo.
Picha zote na Fredy Njeje

Na Dickson Mulashani

Makamu wa Rais wa Serikali ya wanafunzi katika Chuo kikuu cha Dar es salaam Bi. Shamira Mshangama, aliandaa kongamano kubwa lililohusisha watu mbalimbali wakiwemo wanafunzi kutoka shule za Sekondari,wanavyuo,taasisi na asasi za kijamii kwa lengo la kuzungimzia masuala mbalimbali yanayowahusu vijana hasa vijana wa kike na dhana ya uongozi ikiwa ni pamoja na nafasi ya mwanamke katika uthubutu wa kuwa katika nafasi mbalimbali za uongozi.

Akizungumza katika kongamano hilo mgeni Rasmi katika ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh. Sophia Mjema aliwaeleza washiriki wa kongamano hilo safari nzima ya maisha yake katika uongozi lengo likiwa kuwapa mwanga kuwa wanawake wanaweza kushika nafasi mbalimbali bila wasiwasi.

Mh. Sophia aliwaatha vijana hasa wa vyuoni na mashuleni kuto danganyika na kutoa rushwa ya ngono na kuto kujirahisiha maeneo ya kazi ili mtu fulani ampende amchukue ili apate kitu fulani na kusisitiza kuwa hayo ni mambo yanapita na waepuke tamaa hizo.

Kadhalika aliongeza kuwa kwa wanawake wote ambao wanania ya kugombea nafasi kama Ubunge pindi wanapopata wawe mbele zaidi katika kutetea maslahi ya wanawake kwa kuwa wao wanaona mambo mengi zaidi katika jami.

Mwisho alisisitiza kuwa mambo yote yanawezekana endapo amani itadumishwa katika eneo la kazi kwa kuwa sehemu ambayo haina amani hata utendaji wa kazi huwa ni mgumu, alisema kuwa watu wakipendana na swala zima la kazi litakuwa na ufanisi zaidi.     

Kwa upande wake Mkurugenzi mkazi wa Asasi ya kiraia ya Global Peace Foundation (GPF) Martha Nghambi alielezea kwa undani kuwa " GPF ni ni Taasisi isiyo ya kiserikali,ambayo si ya kidini na haitengenezi faida ya aina yoyote ile ina makao yake makuu  katika jiji la Washington DC nchini Marekani na lenye matawi yapatayo 23 duniani kote, yakiwemo mabara ya Afrika,Ulaya, Asia na Marekani ni “Taasisi hii kwa Tanzania ilianzishwa kati kati ya Mwaka juzi 2015 ambapo pamoja na uchaga wake wameonesha juhudi kubwa katika kuhamasisha amani nchini kuanzia ngazi ya familia na jamii kwa ujumla."

Mathalan Mkurugenzi huyo akiongelea umuhimu wa wanawake katika nafasi mbalimbali za uongozi aliwasihi vijana wakike tangu wakiwa wadogo wawe na watu ambao ndio mfano kwao "Role Model" watakao wafanya kutimiza ndoto zao, pia kuwa na uthubutu kwa kuwa wanaweza kushika nyadhifa mbalimbali kuanzia ngazi ya chini mpaka uongozi wa juu.

Nae Mkurugenzi wa  wa Maswala ya Jinsia Chuo Kikuu Cha Dar es salaam Dkt. Kafanabo pamoja na kutoa ufafanuzi wa historia za viongozi wanawake waliowahi kushika nyadhifa mbalimbali nchini Tanzania alisema kuwa nia ya wanawake katika uthubutu wa katika kutafuta nafasi mbalimbali bado hauridhishi kwani safari ya kupambana na mfumo dume hata kwa wanawake wasomi bado ni ndefu

No comments: