Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Maria Mashingo
akipiga chapa ng’ombe katika Kijiji cha Igalula Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa
Katavi leo alipokwenda kuhamasisha zoezi la upigaji na kuwataka wafugaji
kuhakikisha mifugo yote inapigwa chapa ifikapo Januari 31 mwaka huu.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi(Mifugo) Dk. Maria
Mashingo akiwaonesha wafugaji sehemu sahihi ambayo ng’ombe anatakiwa kupigwa
chapa ili kuepuka kuiraribu ngozi baada ya kushiriki zoezi la upigaji chapa
katika Kijiji cha Igalula
wilayani Tanganyika mkoani Katavi leo.
wilayani Tanganyika mkoani Katavi leo.
Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dk. Maria Mashingo
akipiga chapa ng’ombe katika Kijiji cha Igalula Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa
Katavi mapema leo alipokwenda kuhamasisha zoezi la upigaji na kuwataka wafugaji
kuhakikisha mifugo yote inapigwa chapa ifikapo Januari 31 mwaka huu.
Na Kumbuka Ndatta, WMUV
KATIBU Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo)
Dk. Maria Mashingo amewataka wafugaji kuhakikisha wamekamilisha zoezi la upigaji
chapa mifugo yao kabla ya muda ulioongezwa na Serikali wa hadi Januari 31 mwaka
huu kwani baada muda huo kupita haijulikani Serikali itaamua nini kuhusu mifugo
itakayokuwa haijapigwa chapa.
Akizungumza
wakati akishiriki zoezi la upigaji chapa mifugo katika Kijiji cha Igalula Kata
ya Mpanda ndogo Wilaya ya Tanganyika mkoani Katavi, Dk. Mashingo alisema zoezi
hilo la upigaji chapa linatekelezwa kwa
mujibu wa Sheria ya utambuzi ,usajili na ufuatiliaji wa mifugo Na. 12 ya Mwaka 2010 .
Dk. Mashingo alisema upigaji
chapa umelenga kudhibiti magonjwa ya mifugo,wizi wa mifugo, uimarishaji usalama wa afya na mazao ya mifugo sambamba na
kudhibiti usafirishaji na uhamaji wa mifugo kiholela na kuimarisha biashara ya
mifugo na mazao yake kitaifa na kimataifa.
"Wafugaji hakikisheni mifugo yenu yote
inapigwa chapa kwani baada ya Januari 31 mwaka huu hatujui Serikali itaamua
nini kwa mifugo itakayokuwa haijapigwa chapa "alisema.
Dk. Mashingo alisema pamoja nia njema ya
Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuwatetea wafugaji wanaofanyiwa vitendo vya uonevu na
mamlaka nyingine za Serikali pia aliwahimiza kutii sheria za nchi kwa
kutoingiza mifugo yao kwenye maeneo yasiyoruhusiwa kwa mujibu wa sheria.
Pia aliwakumbusha wafugaji kutambua kuwa
rasilimali ya mifugo waliyonayo ina thamani kubwa na kwamba wao pia ni sehemu
ya wawekezaji hivyo ni vyema wakatengeza
miundombinu bora kwa ajili ya mifugo yao kuliko kuisubiri Serikali pekee kujenga
miundombinu hiyo.
“Wafugaji ni wawekezaji muhimu sana katika
nchi yetu kwani kama wasingekuwepo nchi ingelazimika kuagiza mazao ya mifugo
kutoka nje ya nchi na tungelazmika kutumia sh. trioni 17 kwa mwaka”alisema Dk. Mashingo.
Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Cresencia
Joseph amemweleza Dk. Mashingo kuwa mkoa huo
unajumla ya ng'ombe 570,758 ambapo
kati ya hao 423,767 wameshapigwa chapa.
No comments:
Post a Comment