Na Mwandishi Wetu
Mume wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia tiketi ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Amina Chifupa, Bw. Mohamed Mpakanjia amesema yuko fiti (gado) kiafya.
Mpakanjia aliyasema hayo mapema wiki hii alipoongea na mwandishi wetu nyumbani kwake Sinza, jijini Dar es Salaam, kufuatia habari kuwa mfanyabiashara huyo yu hoi na amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
“Ninachuliwa kifo, nimepigiwa simu nyingi na ndugu, jamaa na marafiki zangu, wakihofia afya yangu na nimekuwa nikiwaambia kuwa niko fiti kiafya,” alisema Mpakanjia.
Hata hivyo, mfanyabiashara huyo alikiri kujisikia kuumwa mara baada ya kuandikwa sana kwenye magazeti. “Baada ya kuandikwa na kupokea simu mfululizo za pole, nilijisikia kuumwa, nikaenda hospitali kupimwa, daktari akasema sikuwa na tatizo, nikapewa panado nikarudi nyumbani,” alisema Mpakanjia.
Aidha, mfanyabiashara huyo alisema kuwa alishangazwa na habari zilizoandikwa na gazeti moja la kila wiki (sio la kampuni inayochapisha gazeti hili) kuwa anaumwa na amelazwa hospitali huku akiwa bukheri wa afya.
Licha ya gazeti hilo, mfanyabiashara huyo aliandikwa na baadhi ya vyombo vingine vya habari vikimuelezea kuwa amekumbwa na msongo wa mawazo kutokana na kifo cha mkewe.

2 comments:
naomba utuwekee page ya gazeti la pendwa la IJUMAA nadhani ni la mwezi Juni kiliyoandikwa na SHIGONGO, "WARAKA WA AMINA TOKA KWA SHIGONGO" mana wengi hatukusoma kilichoandikwa tunasikia kwa watu tu juu.
Tunashukuru kwa uamuzi huu wa kutuekea magazeti.
Post a Comment