Saturday, August 4, 2007

Profesa Jay aporwa demu na kizito



Msanii maarufu wa muziki wa kizazi kipya nchini, Joseph Haule ‘Prof. Jay’ anadaiwa kukimbiwa na mchumba wake aitwaye Nice Chande.

Tukio hilo limetokea wiki iliyopita nyumbani kwa mwanamuziki huyo, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa marafiki wa karibu wa Nice ni kuwa, mwanamke huyo amehamishwa nyumba kinyemela na kizito mmoja ambaye yuko karibu sana na kiongozi mmoja wa juu wa chama cha siasa nchini (jina tunalihifadhi).

Habari zaidi zimeeleza kuwa kitendo cha mwanamke huyo kutoweka nyumbani kimemsononesha mwanamuziki huyo na kuathiri utendaji wake wa kazi.

“Kama ulikuwepo Leaders kwenye Tamasha la One Mic utakubaliana nasi kuwa Prof. Jay amechanganywa na mapenzi kwani alishindwa kufanya ‘makamuzi ya kufa mtu’ kama ilivyo kawaida yake,” alisema mmoja wa marafiki hao.

Aidha, inadaiwa kuwa Nice alifika nyumbani kwa msanii huyo baada ya kuambiwa hayupo na kuchukua baadhi ya nguo zake kisha kutoweka.

Mwandishi wetu alimtafuta Prof. Jay ‘ the heavy weight’ na kumuhoji kuhusu madai hayo badala ya kujibu, yeye aliuliza “hayo ni mambo ya siri, wewe umeyapataje?”

Hata hivyo, Prof. Jay alisema kuwa, kwa sasa yuko mikoani akifanya kazi zake za muziki hivyo hajui chochote kinachoendelea nyumbani kwake jijini Dar es Salaam.

Kwa upande mwingine Nice alipopigiwa simu na kuulizwa kuhusu madai ya kutoroshwa na kizito, aliomba apewe muda wa dakika tano ndipo ajibu swali.

Alipopigiwa baada ya dakika tano, aliuliza “hizo habari umezipata wapi na nani amekupa, nakuja huko huko ofisini kwenu uniambie aliyekueleza hayo yote,”alisema.

Prof. Jay amekuwa akiishi na msichana huyo kwa muda mrefu kama wachumba na mara kwa mara wamekuwa wakionekana pamoja katika majumba ya starehe.

Prodyuza maarufu afmaniwa

Produza maarufu wa muziki wa kizazi kipya nchini, Akil Mohamed a.k.a The Brain, hivi karibuni alijikuta akikumbwa na aibu kubwa baada ya kufumaniwa na jimama lake lililojulikana kwa jina moja la Rosemary akiwa na kimwana mwingine.

Tukio hilo la aina yake lilitokea katika Mgahawa wa Steers uliyopo katikati ya jiji la Dar es Salaam ambapo produza huyo alifumwa na mfadhili wake ambaye pia ni mpenzi wake wakiwa katika mahaba mazito.

Waandishi wetu waliokuwepo katika mgahawa huo walimshuhudia Akil akiwa ‘beneti’ na msichana mmoja ambaye hakuweza kufahamika jina lake mara moja.

Akiwa katika mgahawa huo, Akil na binti huyo waliagiza vinywaji baridi na kuanza kunywa lakini ghafla aliingia dada mmoja aliyeonekana kuwa na umbo kubwa ‘jimama’ na kuanzisha varangati kubwa.

“Wewe msh**** umenigandisha nyumbani muda wote kumbe upo huku na kimada wako, utanikoma,” alisikika jimama huyo akilalama.

Rosemary alionekana kufura kwa hasira alimuuliza Akil “huyu uliyenaye ni nani?” Lakini hakupata majibu.

Kufuatia kutojibiwa jimama hilo limfuata Akil na kumnyanyua msobe msobe na kuanza kumshushia kipigo cha nguvu.

Wakati varangati hilo linaendelea, mwanamke aliyekuwanaye Akil alitimua mbio kuelekea kwenye gari walilokujanalo lililokuwa pembeni ya mgahawa huo na kumuacha produza huyo akichezea kichapo.

Hata hivyo, produza huyo alifanikiwa kuchomoka kwenye mikono ya jimama hilo na kukimbilia katika gari na bila kupoteza muda aliliondoa kwa kasi.

Aidha, mwandishi wetu alimshuhudia Rosemary akiwasha gari lake na kulifuata kwa nyuma gari la produza huyo.

Mwandishi wetu hakuweza kufahamu mara moja nini kilitokea huko walikoelekea.

3 comments:

Unknown said...

Herufi zingine hazionekani bro!

Anonymous said...

format maandishi yako ili yasomeke vizuri

Anonymous said...

profesa pole sana kwa kukimbiliwa nampenzi wako jikaze ndio maisha utapata mwingine anyekupenda kwa dhati