Hali hiyo inakuja kufuatia takwimu za hivi karibuni za Tume ya Taifa Kudhibiti Ukimwi nchini (TACAIDS) kuonesha kuwa, kati ya watu kumi waliopimwa, watatu wameathirika na watu hao ni vijana wenye umri wa kati ya miaka 15-49 ambao ndio nguvu kazi ya Taifa.
Aidha takwimu hizo zinabainisha kuwa, kati ya watu milioni 5 waliopima asilimia 7 wameathirika lakini kundi kubwa la wasanii limekuwa likikwepa kwenda kupima afya zao kitendo kinachoashiria kuwa, hawajiamini na afya zao kutokana na mfumo wa maisha wanaoishi.
Hata hivyo, inawezekana hakuna msanii yeyote kati ya wasanii kumi waliotajwa ukurasa wa mbele aliyeathirika lakini, wameshauriwa kwenda kupima afya zao ili waweze kuishi maisha ya uhakika na kuwa mfano wa kuigwa kwa jamii.
Takwimu za hivi karibuni za Shirika la Umoja wa Mataifa linalojishughulisha na masuala ya Ukimwi,UNAIDS zinaonesha kuwa, takribani watanzania wapatao milioni 1.5 wanaishi na virusi vya Ukimwi wakiwemo watu hao maarufu.
Kwa mujibu wa Takwimu hizo, watu milioni 1.3 ya idadi ya wanaoishi na virusi ni wale wenye umri wa kati ya miaka 15-. 45 ambapo wanawake wanaoishi na virusi ni 710,000.
Aidha mtandao wa shirika hilo umetaja kuwa, watoto wanaoishi na virusi vya Ukimwi walio kati ya umri wa miaka 1-14 ni 110, 000 .
Wakizungumza na Ijumaa kwa nyakati tofauti, baadhi ya wataalam wa afya ambao wanajihusisha na zoezi la upimaji Ukimwi kwa hiari linaloendelea nchini, walisema kuwa wameshangazwa na idadi kubwa ya mastaa kutojitokeza kupima afya zao.
Mmoja wa wataalam hao kutoka kituo cha Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini alisema, tangu zoezi hilo limeanza amewapima wasanii wawili tu.
“Wamejitokeza watu wengi kuja kupima afya zao katika kituo hiki lakini kati ya hao nimewapima wasanii wawili tu ninaowafahamu hali inayoonesha kuwa, wengi wao wanalikwepa zoezi hili,” alisema mtaalamu huyo.
Uchunguzi uliofanywa na Ijumaa umebaini kuwa, baadhi ya mastaa wanaambukizwa virusi vya Ukimwi kufuatia tabia yao ya kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja na kubadilisha baada ya muda mfupi.
2 comments:
Choki hawezi kosa kwani alishaua pamoja na Banza-ngoma ngoma
SASA KATI YA HAO WAREMBO NANI KASHINDA??? NINGEPENDA KUJUA.
Post a Comment