Sunday, August 5, 2007

MATUMAINI KWA BINTI SOFIA KUTOKA LONDON!

Sofia, binti mdogo (17), mrembo, lakini anaishi katika maisha yenye mateso sana!



leo asubuhi nimetembelewa katika chumba chetu cha habari na Bw. James (pichani kulia) ambaye ni baba mzazi wa binti Sofia anayesumbuliwa na uvimbe wa ajabu miguuni. Amenieleza kwamba, mara baada ya kutolewa kwa habari kuhusu binti yake katika blog hii wiki 2 zilizopita, amepigiwa simu na watu mbalimbali, na hivi karibuni amepata matumaini ya kupona kwa binti yake kutoka kwa Umoja wa Watanzania waishio London, Uingereza, ambao wameahidi kumsaidia binti yake, seriuosly!

Kwa mujibu wa mwenyekiti wa umoja huo aliyejitambulisha kwa jina moja la Lucas (samahani kama hakuku 'koti' vizuri), Jumamosi ya jana suala hili lingejadiliwa katika mkutano maalum na kuona jinsi ya kuokoa maisha ya binti yake.
Pia kuna msamaria mwema mwingine kutoka Dubai nae ameahidi kumsadia, baada ya kupata maelezo ya kina ya tatizo la binti yake.. shime watanzania tumsaidie binti huyo, naamini inawezekana..... let's change Sofia's life!!


Ifuatayo ndiyo historia ya ugonjwa wa mtoto Sofia na maelezo yaliyotolewa na baba yake mzazi, Bw. James Mwiga, leo asubuhi mbele yangu katika chumba chetu cha habari…....

MIMI Sofia James, nilizaliwa 1990, nina umri wa miaka 17 nilizaliwa mkoani Tabora, wilaya ya Tabora mjini.

Ninaomba msaada wa matibabu ya uvimbe wa miguu yangu, naomba msaada kutoka nchi yoyote itakayo kuwa tayari kunitibu, mimi nakubali endapo nchi yoyote itakuwa tayari kunisaidia. Nasumbuliwa na uvimbe wenye maumivu yapata miaka kumi (10).

MAELEZO MAFUPI ALIPO ANZA KUUGUA SOFIA
Mara baada ya kuzaliwa 1990, mwaka 1998 alianza kupata dalili za uvimbe mdogo miguuni, alipelekwa katika Hospitali mbalimbali Mkoa wa Tabora kwa uchunguzi, lakini hawakubaini tatizo.

Mwaka 2005 hali ilibadilika ghafla baada ya kuvimba sehemu mbalimbali za miguu, mfano wa manundu huku akisikia maumivu makali. Alilazwa kwa muda wa miezi mitano (5) Kitete Hospitali Tabora, kisha akapewa rufaa ya kwenda Muhimbili Government Hospital, Dar es Salaam, Kwa uchunguzi na matibabu zaidi alichukuliwa vipimo Muhimbili na Agakhan Hospital na kuonekana ana tatizo linalojulikana kitaalamu kama Lymphoedema.

Baada ya uchunguzi huo alipangiwa afanyiwe upasuaji awamu sita mara sita kwa siku tofauti, alipangiwa tarehe 04 May 07 apelekwe kwa ajili ya maamdalizi ya upasuaji yaliyopangwa kufanyika tarehe 24-May 07. Alipofikishwa hospitali, madaktari walikaa kikao na kusitisha upasuaji, baada ya kuona mafanikio yatakuwa madogo, wangeweza hatarisha maisha yake badala ya kumuokoa.

Hivi sasa yupo katika hospitali ya Jeshi la Wananchi Tanzania ya Lugalo, jijini Dar es Salaam ambako amepata hifadhi ya kitanda na kusubiri hatma yake, kwa msaada wa Waziri wa Ulinzi, Mh. Juma Kapuya, ambaye ndiye aliyemtoa Tabora.

Kama kuna nchi ambayo itakuwa tayari kumsaidia binti huyu yeye mwenyewe yupo tayari na baba yake yupo tayari( Amekubali).

Kwa mawasaliano zaidi, baba mzazi anawaomba wasamaria wema wote watumie email yangu ya amsalawi@yahoo.com au wawasiliane nae moja kwa moja kwa simu namba: +255 0753 916 690








No comments: