Friday, September 28, 2007

Babu Seya KILIO!


Familia ya mwanamuziki mkongwe nchini, Nguza Viking anayetumikia kifungo cha maisha gerezani baada ya yeye na wanawe watatu kupatikana na hatia ya kubaka watoto miaka kadhaa iliyopita, imepata balaa kubwa.

Balaa lililoikumba familia hiyo na kubainika hivi karibuni na kusababisha vilio kutawala nyumbani kwao Sinza jijini Dar es Salaam ni la mchumba wa Nguza Mbangu aitwaye Melei Yesa Mbombo kuolewa na rafiki yake wa karibu, jambo lililowatia simanzi wanafamilia hiyo.

Kwa mujibu wa mtoa habari wetu ambaye ni mmoja wa marafiki wa familia hiyo aliyeomba hifadhi ya jina lake, mchumba huyo wa Mbangu ameolewa miezi michache iliyopita na mfanyabiashara wa jijini Dar es Salaam anayefahamika kwa jina la Ndama maarufu Mtoto wa Ng'ombe.

No comments: