Friday, September 28, 2007

Mrembo huyu azua balaa!


Picha ya Miss Utalii mwaka 2006 Ania Said, iliyotolewa na gazeti la The Bongo Sun, Jumanne hii, imezua balaa baada ya wasomaji kupiga simu katika ofisi za gazeti hilo wakidai kuwa mrembo huyo hakuwa Mtanzania kama ilivyoainishwa.

Wakizungumza wasomaji wa The Bongo Sun, ambalo ni jipya chini ya Global Publishers, walisema kuwa hawaamini kuwa mrembo huyo ni Mbongo kutokana na mandhari ya eneo alilopigia picha, pozi na mvuto wake.

Aidha waliongeza kuwa, hawatakubali kuwa mrembo huyo ni Ania mpaka pale watakapokutana naye uso kwa uso na kufananisha na picha waliyoiona kwenye gazeti hilo.

No comments: