Mtoto Mathew James, enzi za uhai wake akiwa mikononi mwa mama yake akiomba msaada kwa umma ili kuokoa maisha ya mwanae....ilikuwa Agosti 2, mwaka huu
Mama mzazi wa marehemu Bi Neema (kati) akiaga mwili wa mwanae huku akilia kwa uchungu kabla ya kwenda mazikoni jana.....POMOJA NA JUHUDI KUBWA KUFANYIKA ZA KUOKOA MAISHA YAKE, MTOTO MATHEW AFARIKI DUNIA!
Mama mzazi wa Mathew, Bi Neema, amesema kuwa mtoto wake alilazwa katika hospitali hiyo Septemba mosi akisubiri tarehe ya kufanyiwa oparesheni chini ya uangalizi wa Daktari Sai.
Tarehe 10 Sept, mtoto alipelekwa chumba cha upasuaji lakini ilishindikana kufanyiwa uapasuaji siku hiyo baada ya mishipa yake kutoonekana. Tarehe 17 Sept, siku ya Jumatatu wiki hii, alirudishwa tena na kufanikiwa kufanyiwa operesheni kubwa ambayo ilisaidia kumrudisha utumbo ndani na hapo ndipo tatizo lilipoanza kutokea.
Akizungumza kwa uchungu, Neema alisema kuwa tangu mwanae atoke chumba cha upasuaji, alikuwa akisumbuliwa na vyuma ambavyo viliwekwa sehemu ya haja kubwa.
"Nimehangaika sana juu ya mtoto huyu, Mungu anajua, nawashukuru wale wote walionisaidia kwa hali na mali, Watanzania waliopo Japan, Marekani, Mikoani na Jijini Dar-Es-Salaam, walijitahidi Mathew apone kwa kunichangia, Mungu awajalie sana, ila Mungu ndivyo alivyopenda iwe, uamuzi wake hauna makosa,” aliomboleza kwa uchungu mama mzazi.



No comments:
Post a Comment