Hali ya mauzauza, ilitawala kwenye tukio la kuungua hadi kuteketea kwa Hoteli ya Kitalii ya Sea Cliff, iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam.
Hoteli hiyo ilianza kuungua juzi (Jumamosi), saa 12 jioni na moto kuzimwa saa 4 usiku, ajali ambayo inadaiwa kusababishwa na ‘shoti’ ya umeme.
Mwandishi wetu aliyewasili eneo la tukio muda mfupi baada ya Sea Cliff kuanza kuungua, aliweza kushuhudia mauzauza kwa magari ya zimamoto yapatayo kumi yakishindwa kuzima moto kwa wakati.
Magari hayo, yalipofika eneo la tukio, yalipaki pembeni bila kusjishughulisha kwa chochote huku yakiacha moto ukiendelea kushika kasi na kuzidi kuteketeza hoteli hiyo.
Magari hayo ya zimamoto yalitoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Bandari, Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere, Kampuni ya Knight Support, Ultimate Security na First Responder.
Hata hivyo, haikuweza kufahamika mara moja sababu ya magari hayo kufanya mgomo wa muda, kuzima moto huo, ingawa baadaye yalianza kufanya kazi kwa kasi na kufanikiwa kuuzima ndani ya muda mfupi.
Viongozi waliofika kwenye hoteli hiyo yenye ghorofa tatu, ilipokuwa ikiungua ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Joseph Mungai, naibu wake, Lawrance Masha na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro ambaye aliahidi kutoa tamko lake jana.
Chanzo cha moto huo kilielezwa kuwa ni bomba la kutolea moshi kutoka katika boila ambalo lilitoa cheche ambazo zilimwagika kwenye paa la makuti la hoteli hiyo na kusababisha kuteketea. kama inavyyoneka pichani ukurasa wa mbele.
No comments:
Post a Comment