Monday, September 24, 2007

Mpakanjia afichuliwa aliko!


Mfanyabiashara maarufu chini, Mohammed Mpakanjia ‘Meddy’ ambaye alikuwa hajulikani alipo, sasa amefichuliwa.

Habari za kuaminika kutoka chanzo chetu cha habari zilizolifikia gazeti hili wiki hii, zinasema kuwa Mpakanjia yupo Kimara jijini Dar es Salaam anapumzika. Mtoa habari huyo aliyeomba hifadhi ya jina lake alisema kuwa mfanyabiashara huyo anaishi eneo hilo kwenye nyumba yake nyingine iliyopo Kimara.

Habari zaidi zinasema kuwa hatua hiyo ya kwenda kuishi eneo hilo, inatokana na ushauri wa daktari wake aliyemtaka apumzike kwa muda mrefu. “Unajua alipotoka hospitali alishauriwa na madaktari apate muda mrefu wa kupumzika, hivyo akaamua kuishi Kimara ambako anamiliki nyumba nyingine na watu wengi hawakujui,” alisema mtoa habari huyo.

Chanzo hicho kiliongeza, baada ya uamuzi huo hivi sasa Meddy anapata nafasi nzuri ya kupumzika kama alivyoshauriwa na madaktari wake wa Hospitali ya Lugalo, jijini, alikokuwa amelazwa, kutokana na ugonjwa wa msongo wa mawazo. Hata hivyo, mtoa habari huyo alibainisha kuwa mara baada ya kuruhusiwa kutoka hospitali, marafiki zake walitoa wazo la kumpeleka sehemu ambako angeweza kumpumzika.

“Aliporuhusiwa hospitali baadhi ya marafiki zake walitoa ushauri kwa ndugu zake kuwa akapumzike nje ya nchi kama Uarabuni, Afrika Kusini au Uchina,” alisema mtaoa habari huyo. Habari zaidi zinasema kuwa wazo hilo lilijadiliwa na marafiki hao pamoja na ndugu zake wa karibu, lakini hadi wiki iliyopita hakukuwa na uamuzi uliofikiwa. Imeelezwa kuwa akiwa Kimara, mfanyabiashara huyo anaishi na mke wake Aisha Fat’hi Akrabi na ndiye anayempikia futari kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani.

Mwezi uliopita, Mpakanjia alilazwa katika Hospitali ya Lugalo, jijini Dar es Salaam, akitibiwa ugonjwa wa msongo wa mawazo ambapo baada ya kupata nafuu aliruhusiwa.

No comments: