Lions Club of Dar es Salaam Azania wameguswa na matatizo ya ugonjwa unaomsumbua mtoto Sophia James Mwiga na wamejitolea kusambaza taarifa hizi katika Lions Club mbalimbali duniani ili kuhakikisha mgonjwa huyo anapata matibabu haraka sana iwezekanavyo. Kauli hiyo ameitoa Bi.Alice Phiney Masimba ambaye ni mwanachama wa Club hiyo ya Jijini Dar es Salaam ambaye alifika kumuona mgonjwa huyo wodi namba nane katika Hospitali ya Jeshi ya Lugalo alipolazwa kwa zaidi ya miezi 10 akiwa ameongozana na Bw.Hamza Mikidadi wa Club hiyo. Bi.Masimba ameupongeza mtandao huo kwa kutoa taarifa hiyo kwani imesaidia watu wengi kujua matatizo ya mtoto huyo.nakuamua kumsaidia .
Hadi sasa Sofia yu ngali hospitali anasubiri matumaini ya kumsaidia ambayo mmekuwa mkimpa, majaaliwa yake yako mikononi mwenu!
Hadi sasa Sofia yu ngali hospitali anasubiri matumaini ya kumsaidia ambayo mmekuwa mkimpa, majaaliwa yake yako mikononi mwenu!
No comments:
Post a Comment