Mtaalamu wa nyimbo za kulalamika, Ismail Sadick a.k.a Sumalee, amesema kuwa utumiaji wa vilevi kupita kiasi ndiyo kitu kinachoharibu sauti yake, anaandika Mariam Mndeme.
Ismail ambaye maeneo yake ya kujidai ni Mkoani Tanga Ôwaja leo warudi leo", aliipasha Abby Cool & Mc George Over The Weekend, juma lililopita kuwa kwa sasa ufanisi wake katika kuimba umeshuka kutokana na vilevi hivyo.
Kufuatia hali hiyo, Suma Lee ameahidi kwenda likizo ya muda ili kutotoa wimbo wowote kwa miezi kadhaa kwa lengo la kuruhusu sauti yake ikae sawasawa.
Aidha, aliahidi kuacha kutumia vilevi ili kutetea kiwango chake kisanii kisiporoke sambamba na kutii ushauri wa washkaji zake pamoja na wadau wengine wa muziki ambao mara kwa mara humsisitiza kufanya hivyo.
"Ni hali inayonisikitisha, kiwango changu kimeshuka, sauti yangu sasa inaboa, nikiingia studio sauti inagoma, kwakweli vilevi naacha".

No comments:
Post a Comment