Sunday, September 2, 2007

Street Version

Asilimia 70 ya wapenzi wa soka walikwenda kuangalia uwanja mpya

Muda mchache kabla ya kimuhemuhe kati ya timu yetu, Taifa Stars na Uganda hazijaingia dimbani kunako uwanja mpya na wa kisasa kabisa Dar es Salaam, safu hii ilipiga stori na baadhi ya mashabiki waliofurika kwa wingi uwanjani hapo mwishoni mwa wiki iliyopita.

Swali kwa kila mmoja lilikuwa ni "Wewe kama Mtanzania umekuja uwanjani kufanya nini leo?. Kilichofuata hapo ni majibu kutoka kwa mashabiki hao ambao muda mwingi walionekana wakiwa na furaha ya ajabu.

Baada ya maswali hayo na majibu Street Version ilibaini kwamba asilimia sabini ya mashabiki hao walikwenda kuangalia uwanja, japo kwa upande mwingine walionesha kuipa moyo timu yetu ya taifa. Haya chini ndiyo baadhi ya maoni yao.


Jina: Flora ÔMama Simba
Anaishi: Pugu
Maoni: Hakuna kilichonileta hapa zaidi ya kuangalia uwanja mpya kwani nilipokuwa nauona kwenye picha ulikuwa unanivutia sana ndio maana nikasema sikosi, lazima nije kuangalia. Lakini pamoja na kuja kuangalia uwanja nawapa sapoti wachezaji wetu, ili waweze kufanya vizuri zaidi watakapocheza na Msumbiji.

Jina: Michael Deo
Anaishi: Magomeni
Maoni: Nimekuja kuishangilia timu yangu ya taifa kwasababu mimi ni Mtanzania lazima niipe sapoti pamoja na kungalia uwanja mpya kwani nilikuwa na hamu nao sana. Nilipania sana siku ya kuzinduliwa lazima niwepo, nashukuru mungu nimeweza kutimiza ahadi yangu.

Jina: Paul Solomon
Anaishi: Sinza
Maoni: Mimi kilichonileta hapa leo kwanza ni kuangalia uwanja, kwani hii itakuwa ni kumbukumbu katika maisha yangu na hata wanangu nitawahadithia kwamba ule Uwanja wa Taifa sisi ndio tulioufungua. Kitu cha pili ni kuangalia mechi hii, naawaamini Taifa Stars tutashinda tu.

Jina: Mdugile Juma
Anaishi: Temeke
Maoni: Kitu cha kwanza kilichonileta hapa ni kuangalia uwanja mpya kwa kuwa ni kivutio tosha kwangu, vilvile kwasababu nipo ndani ya uwanja nitaishangilia timu yetu ya taifa.

Jina: Samson John
Anaishi: Sinza
Maoni: Mimi nimekuja kuishangilia timu yetu. Si unajua timu inapocheza nchini kwao inahitaji kushangiliwa kwa sana ili wachezaji wapate nguvu za kutosha na kijiamini wanapokuwa uwanjani. Lakini pia kitu kingine kilichonileta hapa ni kuangalia uwanja mpya kwakuwa nilikuwa na hamu ya kuuona.

Jina: Frebonia Beda
Anaishi: Morogoro
Maoni: Nimekuja kwasababu ya kuuangalia uwanja mpya na kufanya biashara yangu ya kuuza bidhaa ambazo zinawahamasisha watu kuwa karibu na michezo, kama Taifa Stars itafanya vizuri nitaishangilia kwa nguvu zote.

No comments: