Friday, October 26, 2007

SHOWBIZ

Mnyalu (shoto) yuko bize na Madogo.

sanii Mike Mwakatundu Mike T au Mnyalu bado anaendeleza mchakamchaka wa kuwapiga tafu Ômadogo'asanii chipukizi) kupitia studio yake, Mykey Rec iliyopo Mikocheni, Dar es Salaam, Inaletwa kwenu na Frank Kadende.

Ndani ya ShowBiz Mnyalu alisema kwamba kati ya wasanii kadhaa anaofanyanao kazi yumo bwamdogo anayekwenda kwa jina la Lugano Kapakala a.k.a Lugano ambaye kupitia studio yake ameshatoka na kazi yenye jina la Nakupenda ambayo pia imemshirikisha yeye.

'Niliwahi kutamka kwamba ipo siku nitajitoa na kuwasaidia wasanii wadogo, sasa ni wakati muafaka wa kufanya hivyo, nashukuru vijana wako safi na tunaendelea na kazi kama kawa', alisema Mike T.

Kwa upande wake Lugano aliiambia ShowBiz kwamba ana amini muziki unalipa, kitu ambacho kimemfanya aiweke taaluma yake ya ufundi wa kuchomelea vyuma na kuingia kunako muziki ili atoke kimaisha yake.

'Mbali na Mike T, Dully pia amenisaidia sana, niliweza kurekodi katika studio yake, Dhahabu Records kazi inayoitwa Unanidatisha ambayo pia iliniwezesha kupata shoo mbalimbali,' alisema Lugano.

No comments: