Tuesday, October 23, 2007

YOU ARE WHAT YOU EAT!


UKOSEFU WA CHOO:

Chanzo cha maradhi mengine sugu

Watu wengi wanakabiliwa na tatizo la ukosefu wa haja kubwa (choo) na bila wao kuona ni tatizo kiafya. kwa mujibu wa wataalmu wetu wa masuala ya afya, ukosefu wa choo kwa muda mrefu ndio chanzo cha maradhi mengine, kwani wanasema kifo huanzia tumboni (death begins at the colon).

Kwa kuzingatia ukweli huo, binadamu anayeishi na kula chakula kila siku, anapaswa pia kupata choo cha kutosha na cha uhakika kila siku, kinyume chake ni dalili kwamba mwili hauko sawa na ni wajibu wako kuchukua hatua za haraka na za makusudi kuhakikisha unapata haja kubwa bila matatizo.

UKJOSEFU WA CHOO NI KITU GANI?

Kitaalamu, tunaelezwa kwamba ukosefu wa choo (constipation) ni tatizo linalojitokeza kwenye mfumo wa usagaji chakula. Katika hali hii, utumbo unaohusika na kutoa kinyesi hushindwa kufanya hivyo na hata unapotoa, hautoi kwa kiwango kinachotakiwa.

Hali hii inapokuwepo tumboni, ndio huwa chanzo cha magonjwa mengi, kwa sababu kinyesi kinapokaa tumboni kwa muda mrefu hutoa sumu ambayo husambaa na kuingia kwenye mishipa ya damu na kusambazwa sehemu zote za mwili.

Magonjwa kama vile kidole-tumbo, maumivu ya viungo, matatizo ya macho, baridi yabisi, shinikizo la juu la damu na saratani, ni baadhi tu ya magonjwa yanayoweza kuibuka kutokana na sumu inayozalishwa mwilini baada ya mtu kukosa choo kwa muda mrefu.

WENYE TATIZO LA UKOSEFU WA CHOO WANA DALILI HIZI:

Mbali ya kutokwenda haja kwa siku kadhaa kuwa ndiyo dalili kubwa, dalili nyingine alizonazo mtu mwenye tatizo hili ni kuwa na ulimi wenye utandu, kutoa harufu mbaya mdomoni, kukosa hamu ya kula, kuumwa kichwa, kusikia kizunguzungu, kuwa na uvimbe na weusi chini ya macho, vidonda mdomoni, tumbo kujaa, kukosa usingizi na kuharisha baada ya kukosa choo kwa muda mrefu.

TATIZO HILI HUSABABISHWA NA NINI?

Tatizo la ukosefu wa choo huchangiwa, kwa kiasi kikubwa, na kuwa na staili ya maisha na lishe mbovu.

Ulaji wa vyakula visivyokuwa na vitamini na madini, kutokunwya maji ya kutosha kila siku, ulaji mkubwa wa nyama, unywaji mwingi wa chai na kahawa, kumeza chakula bila kutafuna, kula kupita kiasi na kula mchanganyiko wa vyakula usio mzuri pamoja na ile tabia ya kunywa maji wakati wa kula, huchangia kwa kisi kikubwa tatizo hili.

Lakini tatizo hili huchangiwa pia na kuishi maisha ya kukaa (sedentary habits) bila kufanya mazoezi wala kujishughulisha na shughuli yoyote na kupenda kunywa dawa za kuharisha. Pia kuwa na msongo mkubwa wa mawazo kunaweza kukusabisha tatizo hili.

TIBA YA TATIZO KWA KUTUMIA CHAKULA

Kama tunavyooamini siku zote, jinsi ulivyo kunatokana na unavyokula, basi hata tatizo la ukosefu wa choo linaweza kuondoka kwa kula vyakula sahihi na kwa mtindo sahihi, hasa matunda na mboga.

TUNDA LA BELI KAMA TIBA

Tunda aina ya Beli, (Bael Fruit) au kwa jina lingine maarufu Tufaha la Dhahabu (Golden Apple, kama linavyoonekana pichani), ni tunda moja zuri sana kutumika kama tiba ya kuondoa tatizo la ukosefu wa choo. Tunda hili (kwa bahati mbaya sana sijajua kiasili Tanzania linaitwaje, ntaomba mnisaidie) linasifika kuwa bora kuliko matunda yote, hasa linapokuja suala la kutumia matunda kama dawa ya kusaidia mtu kupata choo.

Tunda hili lina uwezo wa kusafisha na kuuupa uhai mpya utumbo.

Itaendele wiki ijayo.

No comments: