Monday, October 22, 2007

Choki, Banza wako tayari kutambulisha!



Ule wakati uliokuwa ukisubiriwa kwa hamu na wapenzi wa muziki wa dansi nchini sasa umewadia. Ishu ni kwamba, wale washikaji waliowahi kujiita mafahari katika albamu yao ya kwanza, wakiwa na Muumini Mwinjuma, wako tayari kutambulisha ujio wao wa pili.

Safari hii ni Ally Choki au Mzee wa majina mengi na Ramadhani Msanja 'Banza Stone' ambao wako tayari kuileta kwenu albamu yao ya pamoja waliyoipa jina la 'Sisi ndiyo sisi', kunako shughuli kubwa itakayokuwa ndani ya ukumbi wa Diamond Jubilee, Novemba 3, mwaka huu.

Ndani ya Abby Cool & MC George Over The Weekend, kwa nyakati tofauti vijana hao walitamka kwamba albamu hiyo tayari imeshatambulishwa na kazi kadhaa ukiwemo wimbo wenye jina la Salary yangu, wakiwa sambamba na Maalim Gurumo ambaye ni mkongwe anayefanyia kazi katika Bendi ya Msondo Ngoma.

MAMBO YOTE DIAMOND JUBILEE, KWANI JIJI ZIMA LITAHAMIA HUKO NOV 3

'Katika albamu hiyo pia tumewashirikisha wasanii wengine wengi na hatutakuwa peke yetu katika uzinduzi huo, bendi kama Akudo Impact, Jahazi Modern Taarab na Wanaume Halisi kutoka TMK watatupiga tafu', alisema Choki ambaye pia aliahidi mabadiliko makubwa katika shoo hiyo.

1 comment:

Anonymous said...

Kuna haja ya kumshauri Ali Choki kuhusu "kifriji" kitamletea matatizo. Inaonyesha yeye anakimaindi kwa sana. Hiyo si afya bali ni kiashirio cha mambo mabaya yanayokuja!