Monday, October 22, 2007

Masanja awabwaga wenzake Ze Comedy


Kutokana na maswali yaliyoambatana na malumbano kwa baadhi ya wapenzi wa sanaa ya maigizo nchini kuhusiana na nani mkali zaidi ndani ya Kundi la Ze Comedy, Street Version iliamua kuifanyia kazi ishu hiyo.

Mwishoni mwa wiki iliyopita iliingia katika mitaa mbalimbali ya Dar es Salaam ili kupata maoni ya nani zaidi kati ya wachekeshaji hao, wanaotikisa Afrika Mashariki na Kati kutokana na uwezo wao mkubwa wa kutoa taswira ya mambo halisi kwa njia ya sanaa ya ucheshi.

Kabla sijaendelea mbele leo hatutakuwa na maoni ya mwananchi mmoja mmoja, badala yake tutajumisha maoni yote na kueleza mchakato mzima ulivyokuwa zikiwemo kura walizopata wasanii hao kila mmoja.

Wakitoa maoni hayo Wabongo wengi walimtaja mchekeshaji Emanuel Mgaya 'Masanja Mkandamizaji' (PICHANI) kuwa ndiye aliyewafunika wenzake wote. Msanii huyo ambaye ameelezwa kuwa na uwezo mkubwa wa kupambanua mambo kwa staili ya aina yake, alijizolea kura 51 kati ya 161 za watoa maoni.

Aliyemfuatia Masanja alikuwa ni Lucas Mhuvile 'Joti' ambaye alijizolea kura 41. Mashabiki waliomzungumzia Joti walisema kwamba, jamaa ni mkali hasa kwa kuzingatia uwezo wake wa kuvaa uhusika wowote na kuumudu ile mbaya, vitu ambavyo huwashinda wasanii wengi.
Nafasi ya tatu ilikwenda kwa Isaya Mwakilasa 'Wakuvwanga' aliyejinyakulia kura 22.

Mshkaji alielezewa kwamba anaweza kuwa mchekeshaji staa popote duniani kwa sababu ya kuonesha kipaji kikubwa katika kuigiza tabia na hulka za makundi mbalimbali ya watu katika jamii ikiwamo wanasiasa na wanawake.

Aliyeshika namba nne alikuwa Mjuni Silvery 'Mpoki' ambaye alijizolea kura 21, akifuatiwa kwa karibu kabisa na McReagan 'Why? Kwanini?' aliyepata 20, wakati Vengu aliondoka na kura 6.

*****************************************

VICE-VERSA Kalapina angefanya kazi gani? Ebwana inakuwaje mtu wetu, namaanisha msomaji, bila shaka uko taiti ile mbaya, mnaendelea kuicheki safu hii. Ni kwamba kupitia hapa mtakuwa mnashiriki kutupa ukweli kuhusu mastaa kibao tutakaokuwa tukiwaandika. Kwa kuanza tunamcheki, kiongozi wa Kikosi cha Mizinga, mshikaji anakwenda kwa jina la Kalama Masoud a.k.a Kalapina ukipenda muite mzawa yaani mjanja wa Dar. Mbali na kufanya vizuri katika game ya muziki wa Hip Hop, mchizi amekuwa akiendeleza ubabe wa kutosha kwa kuwachapa baadhi ya wasanii wenzake na utakapomuuliza kulikoni anafanya hivyo jibu atakalokwambia ni kwamba wamemchokoza. Mshkaji huwa anadai kuwa yeye ni mpole kwa mtu ambaye yuko 'peace' naye. Swali linakuja kwako msomaji, unafikiri Kalapina angekuwa hayupo katika game ya muziki, angestahili kufanya kazi gani? Maoni yenu yatakuwa yakichapishwa katika safu hii kila wiki.

2 comments:

Anonymous said...

Angekuwa JAMBAZI tu hakuna lingine,Mshikaji mshamba fulani hivi ingawaje mwenyewe anajiona mzawa mjanja,ataendekezaje ugomvi?
Kwaufupi Jamaa bado hajakua na ndo maana masuala ya ugomvi anaweka mbele sana kuliko hata hiyo kazi(ambayo ni mziki) inayompeleka chooni.
Binafsi simzimii kabisa anzia yeye hadi kazi yake.

Anonymous said...

Huyu ni haramia kama walivyo wengine tu. Muziki si vurugu, akumbuke kuwa hasira za jamii kuhusu wagomvi kama yeye zina nguvu sana. Amuulize Dudubaya.
Asingekuwa mwanamuziki huyu jamaa angekuwa jambazi.