Akipiga stori na safu hii kwa huzuni, mchizi alitamka kwamba kabla hajafunga safari kuelekea mkoani humo, promota wa ishu hiyo alimfuata Dar es Salaam na kumpa huo mchongo. Kistaarabu walikubaliana kuwa baada ya kumaliza kazi hiyo kubwa kila mmoja avute chake anachostahili.
'Nilimuani sana promota huyo, nikakubali kwenda kupiga naye shoo, lakini baada ya kazi aliingia mitini na pesa zote bila kuniaga, mtu mzima ikabidi nikose muelekeo. Sikuamini kilichotokea kwasababu yeye kama promota alipoamua kutupeleka mkoa inamaana alishajikamilisha, alichofanya ni kujidhalilisha kwa utapeli aliotufanyia', alisema Rhyno.
Aidha msanii huyo aliendelea kusikitika kwamba: 'Kukweli mazingiza aliyotuacha yanasikitisha sana kwani hata nauli ya kurudi Bongo tulikosa, pamoja na hilo, gesti pia tulikuwa tunadaiwa, tulichokifanya ni kuuza baadhi ya vitu vyetu na kurudi Bongo, tuliadhirika sana'.
Rhyno ambaye hivi sasa yuko juu na kazi yenye jina la 'Happy', bado anaendelea kuwakumbusha 'fans' wake kwamba 'Usipime' ambayo ndio albamu yake ya kwanza tayari ipo kamili ikiwa na kazi kama Usipime yenyewe, Namba One, Mistari, Black Chater, The Dan Dada, Usije Niacha, Najua Nimekosea na Kwanini.
No comments:
Post a Comment