Wednesday, February 16, 2011

Fahamu tatizo la ugumba(Infertility)

Ugumba ni hali inayotokea iwapo watu wawili, mwanaume na mwanamke wanapokutana kimwili (au kujamiana) bila kutumia njia yoyote ile ya upangaji uzazi kwa muda wa miezi 12 na kutoweza kushika mimba au kupata ujauzito.

Kuna aina mbili za ugumba;
Ugumba wa asili (Primary infertility) - Hii ni pale ambapo mwanaume na mwanamke hawajawahi kutunguisha mimba kabisa maishani mwao hata baada ya kujamiana au kukutana kimwili kwa muda wa mwaka mmoja bila kutumia njia yoyote ile ya kuzuia kupata mimba.

Ugumba unaotokea baadaye maishani (Secondary infertility) - Hii ni pale ambapo wote wawili, mwanamke na mwanaume wameshawahi kupata ujauzito au kutungisha mimba angalau mara moja maishani mwao na baada ya hapo hawajafanikiwa kupata au kutungisha mimba tena.

Asilimia 30-40 ya tatizo la ugumba huwakumba wanaume na asilimia 40-50 ya tatizo hili huwakumba wanawake, wakati asilimia 10-30 zilizobakia ya tatizo hili husababishwa kwa pamoja na matatizo kati ya wanaume na wanawake, hapa sababu halisi hazijulikani.

Kwa wale wenye afya njema, uwezekano wa kupata au kutungisha mimba iwapo watajamiana mara kwa mara kwa mwezi ni asilimia 25-30. Wanawake hufikia kilele cha kupata ujauzito (peak fertility) wakiwa kwenye miaka ya ishirini.

Mwanamke aliye na umri wa zaidi ya miaka 35 (au baada ya miaka 40) ana uwezekano wa kupata ujauzito kwa asilimia 10.

Je mimba hutungwa vipi? SOMA ZAIDI HAPA: (www.tanzmed.com).


No comments: