Thursday, January 31, 2008

IJUMAA SHOWBIZ

Pauline Zongo asimama na Mzushi

Baada ya kimya cha muda katika game ya muziki wa Bongo Flava, msanii Pauline Zongo ameibuka na kusimama vyema ndani ya kolabo ya wimbo wenye jina la Wapendanao alioshirikishwa na mwanamuziki Charles Lugo a.k.a Mzushi kutoka mkoani Mwanza, Fatma Amri alisema naye.

Ndani ya safu hii, Mzushi alimpa shavu la kutosha msanii huyo kwamba uwezo wake wa kuimba na sauti safi vimeifanya kazi hiyo ikubalike mapema na mashabiki japo ina siku chache tangu iende hewani.

"Huo ni ujio wa albamu yangu ya pili ambayo itakamilika siku chache zijazo, kabla haijaingia mtaani nitaachia kazi nyingine kama Ajira niliosimama peke yangu na Siri ya Mapenzi ambao pia nimemshirikisha Pauline Zongo," alisema Lugo ambaye mashabiki wake tayari wamembatiza majina kibao yakiwemo, Mzee wa Message, Mzee wa Kazi na mengine, huku wakitaka alifute jina la Mzushi.
Huu ndio mzimu wa Imbwiga

ShowBiz imefanikiwa kuipata picha inayoonesha moja ya matukio ya Mzimu wa Imbwiga (pichani juu) katika filamu yenye jina hilo ambayo inatarajiwa kutoka hivi karibuni kupitia Kampuni ya Tollywood ya Dar es Salaam, Violet Mushi anashuka nayo zaidi.

Ndani ya muvi hiyo ambayo tayari imekuwa gumzo karibu nchi nzima, Mzimu wa Imbwiga unaonekana kumsumbua kijana Majani Kasoga aliyecheza kama Bob Kijiti ambaye ndiyo stelingi katika picha hiyo baada ya kukataa kufuata mila na tamaduni za kabila lake.

"Lakini pamoja na kunisumbua kwa kuniangusha mara kwa mara, kunitia uchizi na matukio mengine ya kutisha, bado kuna wakati ulikuwa unanisaidia pale baadhi ya watu walipotaka kunidhuru," alieleza Bob Kijiti alipokuwa akipiga stori na ShowBiz.

No comments: