Sunday, February 3, 2008

BENY: Mimi najipenda tu na wala sio shoga!


Leo tunaye Mtangazaji nyota wa Kituo cha Redio na Televisheni cha East Africa, Benny Kinyaiya.

Mengi yalisemwa kuhusu supastaa huyu wa Bongo, ikiwemo tetesi kibao kuwa eti siyo riziki! Mwenyewe anasemaje? Ungana na Mamu wa gazeti la Ijumaa kama alivyozozanae......

Mamuu: Mambo vipi Ben? Leo Maswali kumi imekutembelea! Unaweza kuwaeleza wasomaji wetu mastaa gani wa ndani na nje ya nchi wanaokuvutia?
Ben: Poa mtu wangu,staa wa nje ninayemzimia kwa sana ni Samuel Etoo na hapa Bongo ninaye lakini kwa kweli sitaki kumtaja.

Mamuu:Unapenda chakula gani maana mwili wako unajengeka vizuri mno?
Ben: Napenda macaron kwa nyama ya kusaga na matunda kwa wingi.

Mamuu: Endapo utafikia wakati wa kuoa ni mke wa aina gani ungependa uwe naye?
Ben: Ningependa nipate mke mwenye akili na atakayenipenda kwa dhati.

Mamuu: Unapenda kuwa na watoto wangapi na mama watoto wako huyo uliyesema unapenda awe na akili na penzi la dhati?

Ben:Watoto watatu wananitosha.

Mamuu: Kwanini unapenda sana Muziki wa Dansi?

Ben: Si kweli, mimi napenda muziki wa aina zote,sichagui ila kwa sababu natangaza kipindi cha Afro Beat ndiyo maana watu wanaweza wakadhani kuwa napenda zaidi muziki huo kumbe siyo!
Mamuu: Je, wewe ni Mtanzania?

Ben: Mimi ni Mtanzania halisi na kabila langu ni Mchaga.
Mamuu: Umetembelea nchi ngapi mpaka sasa?
Ben: Nchi karibu kumi.
Mamuu:Ukiwa kama staa unapata matatizo gani makubwa?

Ben: Mengi sana hasa yale ya kuzungumzwa kwa mabaya.
Mamuu: Umeshawahi kutapeliwa?
Ben: (Huku akicheka) Sijawahi hata siku moja, mi mjanja bwana, tena mtoto wa mjini.

Mamuu: Sasa Ben, tunamalizia na swali la mwisho ambalo ni la kizushi au vingi viulizo. Watu wanasema mengi juu yako. Eti wewe si riziki, kuna ukweli wowote katika hilo?

Ben: (Kwa utulivu na umakini zaidi) Nimeshawahi kuyasikia hayo, lakini ndiyo kama nilivyosema, ukiwa Staa lazima utasemwa kwa mazuri na mabaya, kwa hiyo hayo nayasikia na nayaacha kama yalivyo. Unajua watu huwa na fikra potofu sana, mtu akijependa anatafsiriwa tofauti. Mimi najipenda, napenda kuwa msafi muda wote, kifupi napenda kuonekana mtanashati na maridadi, huo ndiyo utaratibu wa maisha yangu. Wanaofikiria hivyo wanakosea sana.

No comments: