Monday, February 4, 2008

WIKIENDA SHOWBIZ!

Richa: Bora nife masikini

Miss Tanzania 2008, Richa Adhia amesema na safu hii kwamba yuko radhi afe masikini kuliko kujichimbia kaburi kwa kupenda vitu vya bure kama ilivyo kwa warembo wengine, Imelda Mtema alicheki naye.

Mrembo huyo alitamka hayo baada ya kuenea kwa uvumi kwamba, kuna pedeshee yuko radhi kumpa nyumba na gari kama atafanikiwa kutembea naye, kitu ambacho hataki hata kukisikia.

"Bora nife masikini lakini sio kupenda vitu vya bure ambavyo vitaniingiza kaburini, sina tamaa ya kihivyo japo hivi sasa sina mchumba," alisema Miss Tanzania huyo ambaye hakufanikiwa kufanya vizuri katika mashindano ya kumtafuta mrembo wa dunia yaliyofanyika Sanya, China mwishoni mwa mwaka jana.

Akiuzungumzia ukimya uliokuwepo tangu aporejea kutoka China, Richa alisema kwamba ni kwasababu alikuwa hajawekwa wazi na kamati ya Miss Tanzania. "Nilikuwa nawasubiri wanipangie kufanya kazi mbalimbali za kijamii, ".

Aidha, mrembo huyo alisema kwamba, pamoja na kuwepo kwa tetesi hizo za kutafutwa na mapedeshee, tangu ashinde taji la Miss TZ hajawahi kusumbuliwa na mwanaume yeyote, zaidi ya kusikia kwa watu tu.


H. Baba achefuliwa na nyodo za Wakongo

Msanii Hamis Ramadhani Baba "H. Baba", hivi majuzi aliibuka na kutamka kwamba nyodo zinazofanywa na baadhi ya wanamuziki wa Kongo wanaofanya kazi Bongo zinamkera ile mbaya, Richard Bukos aliinyaka hiyo.

Msanii huyo anayetumia staili ya "Poteza" alitamka hayo muda mchache baada ya kushuka jukwaani katika ukumbi wa New Msasani Beach Club, Dar es Salaam akitokea kuwasapoti vijana wa Akudo Impact.

"Akudo pekee ndiyo bendi iliyo na Wakongo wengi ambao hawana nyodo, inawakaribisha wasanii mbalimbali jukwaani ambao huonesha vipaji vyao, tofauti na bendi nyingine zenye wasanii wa asili hiyo," alisema H. Baba.

1 comment:

Anonymous said...

Sasa Richa aelewe kuwa hana uzuri wowote,mwanamke wa kweli mrembo na mzuri hasa wa kuwa miss TZ lazima upatwe na usumbufu kutoka kwa watu wanaojaribu bahati zao juu yako,km hupati ujue huna uzuri wowote dada tena pole yako,siyo lazima uwakubalie lakini hata wa kukusumbua huna!!!!rudi kwa GURU dada akakuague si bure mdogo wangu.