Thursday, February 7, 2008

SAKATA LA RICHMOND JIONI YA LEO BUNGENI!

Nukuuu za wabunge bungeni:

Mh. Spika nimetafakari kwa kina sana jambo hili, nikajiuliza kulikoni mpaka watu wazima wakakaa na kuamua kufanya haya…nimetafakari sana na kugundua haya yote ni Uwaziri Mkuu…it is their wish which am going to grant…Mh. Spika nimetafakari sana jana usiku juu ya jambo hili, nimeamua kumuandikia Mh. Rais barua ya kujiuzulu….!” Mh. Edward Lowassa


“Yesu hakutenda dhambi lakini alihukumiwa..” Karamagi


“Siogopi kuwajibika kwa maana hiyo…lakini mkimsingi mimi ni mtu ninayeheshimu uwajibikaji…namuomba Rais kujiuzulu…” Dk. Msabaha

“Karamagi ni rafiki yangu, Msabaha ni rafiki yangu, lakini katika hili sina urafiki na mtu, hata angekua Malecela (mumewe)……”, Mh. Mama Anna Kilango (CCM).


Richmond ni wahuni tu, ina kiofisi cha Internet tu pale karibu na hoteli yangu ya Keys Hoteli, siju Serikali iliwaokota wapi wahuni hawa…,katika nchi kama China, watu hawa sio tu wanajiuzulu, wananyongwa hadharani…” Mh. Ndesamburo
(CHADEMA).


“Mikataba yote sasa iletwe bungeni ijadiliwe…ianzishwe kamati ya kufuatilia kauli zinazotolewa na serikali hapa bungeni……kila aliyehusika atetemeke aondoke humu ndani..hatuna mzaha..” Mh. Kilonsi Mporogomi (CCM).


“Naamini mnapata maombi ya Mchungaji Rwakatare, unaongea kama una nguvu za Mungu…(kicheko)…” Mh. Spika Sitta akimtania Mh. Mporogomi baada ya hotuba yake.


“Hawa Takukuru sijui wafanywaje sasa…
kama tunatetea maslahi ya wananchi tusiogope, tutee kabisa..hali imekuwa mbaya kwa wananchi wa chini..lakini tatizo ni hawa Richmond, bei ya umeme imekuwa kubwa sana..” Mh. Yono Kivela (CCM)

No comments: