Tuesday, July 8, 2008

MAAJABU YA ASALI

You are what you eat!
Licha ya sifa yake ya kuwa na utamu wa asili usio na madhara hata kwa wagonjwa wa kisukari, asali pia ni tiba ya magonjwa mengi, pia ni kinga ya maradhi yanayosababishwa na bakteria, fangasi na mengine mengi. Asali mbichi ndiyo bora zaidi kuliko iliyopikwa.

ASALI DAWA YA KIFUA KWA WATOTO
Uchunguzi wa hivi karibuni uliofanywa na Chuo kimoja cha dawa nchini Marekani, (Penn State College of Medicine), ulithibitisha kuwa asali inaweza kutibu magonjwa ya kifua, kikiwemo kikohozi kwa watoto wenye umri kuanzia miaka 2-18. Hivyo kwa mzazi kujenga mazoea ya kuwapa asali wanae ni jambo la busara.

ASALI DAWA YA KISUKARI
Ingawa watu wenye kuugua ugonjwa wa kisukari (type 2) huwa hawaruhusiwi kula vyakula vyenye sukari, lakini wanaweza kula asali kwani ni dawa kwa njia moja ama nyingine, kutokana na kuwa na virutubisho aina ya ‘fructose’ na ‘glucose’ ambavyo vinahusika na udhibiti wa kiwango cha sukari kwenye damu ambavyo havina madhara.

Aidha, inaelezwa kuwa ili ini lifanye kazi yake vizuri, linahitaji ‘mafuta’ ya kuendeshea na mafuta ya ini yanapatikana pia kwenye asali, hivyo kwa kutumia asali iliyo bora utaweza kuimarisha utendaji kazi wa ini na hivyo kujiepusha na matatizo ya kiafya ya ini.

ASALI HUONGEZA KINGA YA MWILI
Asali pia inaelezwa kuwa na uwezo wa kuongeza kinga ya mwili. Utafiti uliofanywa katika hospitali kadhaa nchini Israel ulionesha mafanikio hayo kwa aslimia 64 ya wagonjwa waliopewa asali katika utafiti huo na hata asilimia 32 ya wagonjwa wa kansa nao walionesha matumaini mapya ya maisha baada ya kutumia dozi ya asali.

ASALI DAWA YA VIDONDA
Tangu enzi na enzi, asali imekuwa ikitumiwa na mababu zetu kama chanzo cha nishati ya mwili, lakini pia katika utafiti wa hivi karibuni, imegundulika kuwa asali ina ewezo mkubwa sana wa kuponya vidonda vya aina mbalimbali kutokana na viambata vyake kuwa na uwezo wa kukausha maji haraka kwenye kidonda.

Aidha, virubisho vingine vilivyomo kwenye asali vina faida kubwa kwa wana michezo kwani huongeza nguvu na wana michezo wengi wamekuwa wakitumia vyakula vitokanavyo na asali au vyenye mchanganyiko wa asali na wameona mafanikio makubwa.

KIJIKO KIMOJA CH ASALI KINGA YA SIKU NZIMA
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa hivi karibuni, asali ina uwezo wa kutoa kinga dhidi ya vidudu nyemelezi ambavyo husababisha magonjwa mbalimbali mwilini pale mwili unapokuwa hauna kinga. Hivyo kijiko kimoja cha chakula cha asali kikitumiwa kila siku huwa kinga tosha (antioxidants).

Kutokana na ubora wa asali, watu wenye ugonjwa wa kisukari aina ya pili (Diabetes 2), wanapotumia asali, utafiti unaonesha kuwa kiwango chao cha sukari kwenye damu hushuka na hivyo kushauriwa kutumia asali kwenye chai na milo yao mingine badala ya sukari nyeupe.

Kwa ujumla asali ina faida nyingi katika mwili wa binadamu, kwani ni chanzo kikubwa cha vitamini na madini. Inaelezwa kuwa asali ni chanzo kizuri cha vitamin B2, B6, madini ya chuma na manganizi (manganese). Anza sasa mazoe ya kula asali, ila hakikisha una pata asali halisi, siyo feki.

4 comments:

Anonymous said...

Sasa huku ulaya nilipo kuna asali ya maua, na asali ya nyuki. Sasa nitajuaje ipi ni sahihi?

Mrisho's Photography said...

Labda ningependa kujua kwanza hiyo asali ya maua ni artificial, yaani inatengenezwa na binadamu au ni ya asili inayotengenezwa na nyuki mwenyewe. kama inatengenezwa na binadamu siwezi kusema ni nzuri au mbaya labda nijue ingridients zake, lakini kama inatengenezwa na nyuki mwenwewe bila shaka ni bora. lakini kwa ujumla asali itokanayo na nyuki ndiyo bora na ina mchanganyiko wa maua na vitu vingine vya asili ambavyo havina madhara kwa binadamu.

Anonymous said...

Did you know that asali ( natural one ) is the ONLY food that does not go bad or expire ?

Its a fact.

Anonymous said...

pia asali ikiwekwa kwenye deep freezer haigandi hata siku moja... lakini pia hata ukiiweka tu mahali pa kawaida haiharibiki