Monday, October 27, 2008

WIKIENDA SHOWBIZ!

The Game
MTV Award: Prof. Jay uso kwa uso na The Game

MTV Awards ikishirikiana na Kampuni ya Global Publishers, inakuhabarisha kuwa, Novemba 22 katika jukwaa la The Velodrome, Nigeria mwakilishi wa Tanzania kunako tuzo za MTV Afrika, Joseph Haule ‘Prof. Jizze’ atakutana uso kwa uso na mchizi kutoka pande za Marekani, The Game ambaye ni mpinzani wake, Rebeka Bernard anakuhabarisha.

Ndani ya safu hii, Jay alisema kwamba, anaamini itakuwa siku nzuri na ya kukumbukwa kwake kwani atawashangaza Wanigeria na watu wengine watakaohudhuria sherehe hizo pale atakapoibuka na ushindi kwa kuwapoteza kina The Game na Lil Wayne ambaye pia anawania tuzo hiyo, (Msanii bora wa Hip Hop).

Ili kumuwezesha Prof. Jizze afanikiwe kuibuika na tuzo hiyo, anaomba umpigie kura kwa kuandika neno Hip Hop E kwenda namba 15555. Kura yako ndiyo itakayompa jeuri ya kuwafunika mastaa hao wa Marekani, bila kuwasahau wasanii wengine wawili, 9ice kutoka Nigeria na HHP wa Afrika Kusini.

Ishu zaidi kuhusiana na tuzo hizo pamoja na mjumbe wetu, Prof. Jay endelea kucheki na sisi kupitia Magazeti yanayochapishwa na Kampuni ya Global Publishers, kusikiliza Radio Clouds pamoja na kuangalia Televisheni ya TBC 1.
*******************************************************************************

FA
TMK
AY

TMK Family, A .Y, Mwana FA, Z-Anto kuiwakilisha Bongo Tuzo za Kisima

Kutoka wilayani Temeke, Dar es Salaam, ShowBiz imedondoshewa ishu kwamba, Kundi la TMK Family limetajwa kuiwakilisha Bongo kunako Tuzo za Kisima ambazo hutolewa nchini Kenya kila mwaka.

Meneja wa kundi hilo, Said Fella alisema na safu hii katikati ya wiki hii kwamba, kupitia ngoma yao, Dar Mpaka Moro wametajwa kuwania tuzo ya wimbo bora kutoka Tanzania.

“Mbali na wimbo bora, pia tumetajwa kuwania tuzo ya kundi bora tukichuana na wasanii wengine wa Bongo. Tunawaomba mashabiki wetu na Watanzania watuwezeshe kuiletea sifa nchi yetu kwa kutupigia kura, waandike neno Kisima, wanaacha nafasi, wanaandika 22E, kisha watume kwenda namba 15550, hiyo ni kwa wimbo bora.

“Ili kundi letu lishinde, waandike neno Kisima, wanaacha nafasi, wanaandika 31C, kisha watume kwenda namba 15550. Tunaamini mashabiki ndiyo waliotufanya tuwe hapa na kutajwa kuwania tuzo hizo, hivyo hawatatuangusha,” alisema Fella. Wasanii wengine waliotajwa kuwania tuzo hizo ni pamoja na A.Y na Mwana FA ambao namba yao ya kuwawezesha ni Kisima 25B kwenda 15550, Z-Anto na video ya Binti Kiziwi (Kisima 25 E kwenda 15550) na Kassim na wimbo wake haiwezekani (Kisima 22D kwenda 15550).


No comments: