Thursday, July 23, 2009

LISHE NDIYO KILA KITU KWA MWENYE VIRUSI

You are what you eat
Katika makala zetu zilizopita, tuliwahi kuandika kuhusu dhana nzima ya Ukimwi na kusema kuwa Ukimwi siyo ugonjwa bali ni hali. Tulifafanua kuwa maana ya UKIMWI ni ‘dalili’ ya Upungufu wa Kinga Mwilini na siyo ugonjwa kama baadhi ya watu wanavyodhani.

Aidha, tulisema kuwa, kwa tafsiri hiyo ya UKIMWI, ina maana kwamba kila mwenye UKIMWI siyo lazima ana VIRUSI vinavyosababisha Upungufu wa Kinga Mwilini na kila mwenye VIRUSI (HIV Positive) siyo lazima ana UKIMWI. Hii ni dhana pana ambayo ikieleweka vizuri, umuhimu wa lishe mwilini nao utaeleweka vyema.

Katika mfululizo wa makala haya yatayoanza leo, tutaangalia ni kwa nini lishe ndiyo kila kitu kwa mtu anayeishi na virusi vinavyosababisha UKIMWI. Nimepata maombi mengi kutoka kwa wasomaji wetu wakitaka pia tuwakumbuke wenzetu wanaoishi na virusi vya Ukimwi kwa kuwakumbusha lishe sahaihi itakayowasaidia kuwapa kinga imara dhidi ya maradhi nyemelezi.

Kwa nini lishe bora ni muhimu zaidi kwa wenye virusi?
Lishe bora ni muhimu kwa wenye virusi vya Ukimwi kwa sababu hufanya mfumo wa kinga mwilini kuwa imara, hivyo kuusaida kupambana na maradhi ipasavyo. Pia lishe bora huboresha maisha. Lishe bora ni haki na wajibu wa kila mtu, hata kwa wale ambao hawajaathirika.

Bila lishe bora, matatizo ya kupungua uzito, kwashakoo yataendelea kuwa mambo ya kawaida, licha ya kutumia dawa za kuongeza kinga, na hali hiyo inaweza kuchangia kupatwa na magonjwa mengine hatari. Halikadhalika, lishe bora hufanya dawa unazokula zifanye kazi sawaswa.

Aidha, lishe bora pamoja na mazoezi, huweza kuondoa dalili za magonjwa kama vile kuharisha, kusikia kichefuchefu, kutapika, kusikia uchovu, shinikizo la damu na kisukari.

Hivyo basi, ili mtu mwenye virusi na ukimwi aweze kuendelea kuishi maisha ya afya, ni lazima azingatie lishe hiyo bora. Pengine mtu utajiuliza, lishe bora ni ipi na unawezaje kuijenga? Hapa tunakuelimisha ifutavyo:

LISHE BORA NI IPI?
Lishe bora ni ile inayotokana na vyakula vya mboga mboga, matunda, nafaka halisi na vyakula jamii ya maharage, pamoja na vyakula vya protini vyenye mafuta kidogo. Vyakula tajwa hapo juu vina kiwango kikubwa cha virutubisho na vina mchango mkubwa sana kwenye ustawi wa afya yako kuliko vyakula vitokanavyo na sukari na mafuta pekee.

DONDOO ZA KUJENGA LISHE BORA
Kila siku hakikisha unakula mboga mboga na matunda ya kutosha, kwa nyakati tofauti, kiasi cha milo mitano hadi sita, sawa na vikombe vitatu. Kula mboga na matunda mchanganyiko ya rangi tofauti.

Kwa kuwa vyakula vya wanga (carbohydrates) ndivyo vinahimizwa kuliwa kwa wingi kwa mtu mwenye virusi, vyakula utakavyokula kwa siku, asilimia 50 vitokane na nafaka halisi (ugali wa mahindi yasiyokobolewa, mtama, ngano, uji wa ulezi, n.k).

Kula vyakula vya kuongeza protini mwilini ambavyo havina mafuta mengi, kama vile nyama ya kuku (bila ngozi), samaki, nyama steki isiyo na chembe ya futa (lean-meat) na bidhaa zitokanazo na maziwa yasiyokuwa na mafuta (low fat au fat free milk).

Punguza ulaji wa vyakula vyenye sukari nyingi, vyakula vitamu-vitamu na vinywaji baridi, kama vile soda, kwani vina virutubisho vya kutosha na huchangia kuamsha kiwango cha sukari mwilini.

Kila siku kula vyakula vingi vitokanavyo na mbegu mbegu, kama vile karanga, korosho na vyakula jamii ya maharage, kunde, njegere, n.k.

KWA NINI UNYWE MAZIWA YASIYO NA MAFUTA?
Itaendelea kesho

4 comments:

Anonymous said...

mimi napenda kuku uliza unaweza kula maandazi juicy au yogurt maana ndio vitu sielewi vinafaa na mziwa ukinywa yoyote kwanikuna tatizo gani mayai je nisaidie ili nijue.

Mrisho's Photography said...

unaweza kula, lakini kwa kiasi kidogo, siyo vitu vya kupenda kula kwa wingi na kila siku..kula kiasi tu na ule kwa wingi vyakula tulivyovieleza kwenye makala haya...asante.

Anonymous said...

kwani juicy si ni matunda mbona unasema tusinywe kwa wingi na juicy ni 100% ya matunda sawa nimekuelewa lakini ni napenda kuwa na uhakika.

Anonymous said...

Hvi m2 aliyepungua mwili kwa ukimwi anaweza kuwa mnene tena? Alafu nawezake kuondoaje hali ya kukosa hamu ya kula