KISA MKASA.....
Bwana Juma alikopa hela katika benki moja jijini dare s salaam zaidi
ya milioni 10 , moja ya masharti ya mkopo huo ni kwamba lazima pesa
hizo zihifadhiwe katika benki hiyo hiyo , na kweli bwana juma alifanya
kama benki ilivyomtaka afanye baada ya wiki moja bwana juma alienda
katika mashine moja ili atoe pesa kidogo kiasi cha shilingi laki
2 ,siku 4 zilizofuatia akaenda kutoa kiasi kama hicho tena , siku 4
tena zilizofuatia akaenda kuchukuwa pesa kutumia mashine hizo akakuta
pesa zake hakuna katika account yake .
Bwana juma hayuko mwenyewe katika kuuliza uliza kwa wateja wengine nao
wakamwambia pia pesa zao zimepotea katika mazingira ya kutatanisha
wakati wanachukuwa pesa katika mashine za ATM , bwana Juma alivyoenda
kuripoti suala hili katika benki husika akaambiwa kwamba inaonyesha
alichukuwa pesa nyingi zaidi katika mashine hizo za ATM siku hizo za
Jumamosi na Jumapili Jioni.
Kumbuka wizi mkubwa katika mashine za ATM unatokea Jioni haswa siku za
mwisho wa wiki , katika siku hizi pia ni ngumu kuwasiliana moja kwa
moja na benki yako kama tukio hilo limetokea papo kwa papo wataweza
kukuambi uende siku za kazi ,ili waweze kushugulikia vizuri tatizo
lako sio kuibiwa pesa tu hata ukidondosha Kadi yako ya ATM mfano pia
ni ngumu kupata mawasiliano ya moja kwa moja na banki hizi mpaka siku
za kazi .
…………………………………………………………………………….
Ukisoma Gazeti la mwananchi la leo kurasa ya mbele wameonyesha mfano
wa jinsi mashine za ATM zinavyotakiwa kuwa pale mteja anapoenda
kuchukuwa pesa katika mashine hizo na pale ambapo vifaa maalumu ya
kuhifadhi taarifa za mteja vinavyoonekana vikichomekwa katika mashine
hizo za ATM .
Kulingana na Gazeti la mwananchi inawezekana bwana Juma hakupewa
mafunzo ya kuweza kutambua mashine za benki zake za kutolea pesa
zilivyo na kama kuna badiliko lolote limetokea katika mashine hizo
bwana juma hakupewa taarifa na benki husika au pengine yeye binafsi
hakutaka kuuliza , au kudadisi utofauti wa mashine mbali mbali za
ATM .
Naamini benki zote huwa na taarifa zote muhimu kuhusu wateja wao ,
kuanzia picha , namba za simu , anuani za barua pepe na mawasiliano
mengine , chochote kikitokea ndani ya benki basi ni wajibu wa benki
kutoa taarifa kwa wateja wake , mfano kama kuna suala la kufunga vifaa
maalumu katika ATM za benki hizo kunakofanywa na wahalifu hawa kama
benk ingekuwa inajua hivyo ingawataarifu wateja wake pamoja na kuweka
picha za mashine za ATM zilivyo na kama kuna badiliko lolote
wajulishwe .
Sasa je hawa wahalifu wanajuaje mfumo wa ATM ? kwanini mhalifu
anaendakatika mashine ya ATM na kuweka kifaa kiurahisi hivyo bila hata
ya Mlinzi kuwa na mashaka nae ina maana vifaa hivi ni vya kufungwa tu
katika sekunde au dakika kadhaa chache mlinzi anakuwa umbali gani na
mashine hizo za ATM hata asiweze kujua kama kuna kitu kipya
kimefungwa ?
Watu wanaoweza kujua mifumo ya mashine hizi ni Wafanyakazi wa Benki ,
wafanyakazi wa kampuni zinazofanya matengenezo katika benki hizo au
zile zilizofunga mashine hizo na sio zaidi ya hao , mtu kuja kufunga
kifaa au vifaa atakuwa kapata taarifa muhimu kuhusu mashine hizo toka
kwa watu hao hapo juu , katika taarifa za gazeti zinasema watu hao ni
raia wa Bulgaria , Katika mashine hizo lugha zinazotumika ni
Kiingereza Na Kiswahili je sisi tuna uhusiano Gani na Bulgaria ? wao
hizo sio lugha zao kuu inawezekana wanapata maelekezo toka watu wa
ndani kwamba kitu Fulani kina maanisha hivi na vile .
Je benki hizi zinatabia za kufuatilia wateja wao kujua tabia Fulani
Fulani kuhusu wateja hao wakati wanachukuwa pesa , najua nchi kama
Nigeria kuna kampuni zimeajiri watu kwa ajili ya kufuatilia wateja wao
katika sehemu nyingi wanazoshugulika na pesa zao kama chochote
kikitokea inakuwa rahisi kufanya maamuzi kutokana na anavyofuatiliwa
na vijana hao ndani ya benki husika au nje ya benki na kampuni ambazo
ziko huru kiutendaji .
Halafu kuna hili suala la mporomoko wa Uchumi duniani , inawezekana
hii hali imechangia kwa kiasi kikubwa kwa benki nyingi kuingia katika
matatizo na wizi wa pesa za watu ndani ya benki , je inawezekana
kwamba kuna mpango maalumu kati ya baadhi ya wenye benki na pesa
zinazoibiwa yaani watu wanakopeshwa pesa hizo hizo zaidi ya miamoja
ili waweze kutengeneza faida haraka haswa kwenye benki ambazo sio za
nchini ? hili pia linawezekana kufanyike uchunguzi tu kuna benki
zinajaribu kudanganya wateja wake kwa njia hii .
Mwisho , suala hili lipo na linaendelea je raia haswa wateja wa benki
hizi wameandaliwaje kupambana na uhalifu huu ? je wachukuwe pesa zao
zote benki au wafanyaje wamepewa njia gani mbadala za kuweza kupamba
na suala hili ? vyombo vyetu vya usalama navyo vinapambana vipi na
suala hili sio lazima vipewe hints na raia wema vinatakiwa navyo
vijipange sehemu mbali mbali kuweza kufuatilia watu hata kujiingiza
kwa makusudi katika makundi ya uhalifu huu kuweza kuwatambua .
***************
By Yona Maro

No comments:
Post a Comment