Tuesday, July 21, 2009

Ras Makunja na Ngoma Africa aka FFU katika makamuzi Fest-Africa, Finland


Mwanamziki Ras Makunja aka Bw.Kichwa Ngumu na mzimu wake FFU ,juzi jumamosi walifungua ukurasa mpya katika jukwaa la Fest-Africa,kwani waliweza kuwapa burudani ya aina washabiki wa ufini, wanamziki washambuliaji (FFU) wa safu ya mbele waliweza kuwamdudu washabiki vizuri,Ras Makunja kiwaongoza jukwaani washambuliaji wake wa safu ya mbele mpiga solo Chris-B,ambaye pia anaimba na Bi.Severne aka Sevasha au afande wa kike,huku mdundo mkali wa The Ngoma Africa Band ukiwasindikiza na kuweza kufanikiwa kuwayumbisha washabiki katika onyesho hilo! Kitu cha kufurahisha mziki huo wa Ngoma Africa uliweza kuwazoa washabiki na kupanda jukwaani kusakata ngoma za moto! mojawapo ya walivutwa jukwaa ni "Mzee Mponda" au tumwite "Dady Mponda" alipanda jukwaani na akawashangaza maelfu ya washabiki kuwa "kuwa wazee wa Kiafrika" wanajua kucheza mziki na kutoa ushindani kwa vijana! wasikilize ngoma afrika hapa http://www.myspace.com/thengomaafrica
(imetumwa na mdau mwenyewe)

1 comment:

Anonymous said...

jamaa mkali!anaweza kulimudu jukwaa si mchezo